Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 7 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa majadiliano na muda uwapo na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Ibada hii inazingatia wazo la mapenzi ya kiungu, kwa kuzingatia karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo iliyotajwa katika Ufunuo 19. Wazo la ndoa kama namna ya kuwasilisha uhusiano wa Mungu na watu wake, na mwaliko kwa wote kuja na kuwa sehemu ya jamii inayounda bibi-arusi wa Kristo ni ujumbe mkuu katika ufunuo wa kibiblia. R. C. Ortlund, Jr. anazungumzia picha hii ya Kristo kama bwana-arusi na mume kwa watu wa Mungu, Kanisa, wakati wa utimilifu wa mambo yote yaliyotajwa katika andiko kuu la mwisho la Ufunuo. Akizungumzia matukio yaliyotokea mbinguni baada ya kuangamizwa kwa kahaba mkuu, Babeli, Ortlund anadokeza kwamba: Baada ya Babeli, yule ‘kahaba mkuu aliyeiharibu dunia kwa uasherati wake’ (Ufu.19:2) kuhukumiwa na Mungu, watakatifu washindi wanashangilia kwamba ‘arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari’ (Ufu. 19:7). Amepewa kuvikwa ‘kitani nzuri, ing’arayo, safi’ kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu (Ufu. 19.8). Mume wa bibi-arusi anajiletea Kanisa kwake kwa adhama, bila doa au kunyanzi au kitu chochote cha aina hiyo (taz. Efe. 5:26-27). Uhalisia wa ufananisho huu hatimaye unaonekana wakati Yerusalemu mpya inaposhuka kutoka mbinguni kwa Mungu, iliyotayarishwa kama bibi-arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe (Ufu. 21:2). Hakutakuwa na ndoa za kibinadamu mbinguni (Mk. 12:25), kwa maana mbingu ndio itakuwa ndoa. Ni vigumu kujadili hili bila kutumia nathari ya hali ya juu zaidi, kama Jonathan Edwards anavyoonyesha (*Works [Edinburgh, 1979 reprint], toleo la 2, uk. 22): Kisha kanisa litaletwa kwenye furaha kamili ya bwana-arusi wake, likifutwa machozi yote katika macho yake; na hakutakuwa na umbali au kutokuwepo tena. Kisha ataletwa kwenye karamu za arusi ya milele, na kukaa milele pamoja na bwana arusi wake; ndio, kukaa milele katika kumbatio lake. Ndipo Kristo atampa mapendo yake; naye atakunywa na kushiba, naam, ataogelea katika bahari ya upendo wake . Kwa muhtasari: muundo wa jumla wa mafundisho

1

 2 Ukurasa wa 372 Ibada

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online