Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 7 5
ya Biblia juu ya ndoa unafichua ulinganifu wa mfano kutoka Mwanzo hadi Ufunuo, kama ambavyo ‘mwili mmoja’ kwa ndoa ya binadamu, takatifu lakini ya muda, unaelekeza mbele juu kwenye muungano wa milele wa kiroho wa Kristo na bibi arusi wake, Kanisa. Ishara iliyo katika ndoa ya kidunia inaupa uhusiano huo heshima kubwa; umuhimu wake unakwenda zaidi ya mambo ya kibinadamu na ya muda hadi mambo ya kiungu na ya milele. ~ R. C. Ortlund, Jr. “Marriage.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. Hapa Ortlund kwa usahihi na kwa ufupi anatoa muhtasari wa nguvu ya taswira ya ndoa kuingia katika hadhi na ukuu wa ndoa ya kimungu, matokeo ya mapenzi matakatifu ambayo Mungu amekuwa akikuza na watu wake tangu mwanzo wa wakati. Kile ambacho Jonathan Edwards anarejelea kama “karamu ya arusi ya milele”, na kile Ortlund anachorejelea kama “muungano wa milele wa kiroho” ni marejeleo yanayohusu taswira ya ndoa. Hata hivyo tunapaswa kuelewa taswira hii ya kuvutia; tunajua kwamba watu wa Mungu ama kwa hakika watafurahia ukaribu wa milele na Bwana, na kwamba uhusiano huu unafananishwa na mahaba na ndoa ya duniani. Tunapata kina cha uhusiano kupitia ishara, sio nje yake. Mungu anatualika kutafakari maana ya uhusiano katika mwangaza wa ishara, na, kwa kufanya hivyo, tutaweza kufahamu katika viwango vipya umuhimu wa muungano wetu na Kristo kama washiriki wa mwili wake, yaani Kanisa. Mifano hii (kama ambavyo mifano yote katika somo hili inavyoakisi) imeundwa ili kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na masuala ambayo ama yalitokana na hali halisi, au ni simulizi za kutunga kulingana na hali halisi za maisha. Kwa maana moja, mifano huwapa wanafunzi fursa ya kutumia moja kwa moja na kwa nguvu maarifa yao juu ya kile wanachojifunza, na kufanya majaribio katika aina ya kufikiri ambayo ni muhimu katika kuchukua ukweli kutoka kwenye mazingira ya kinadharia hadi ya vitendo. Tumia muda mzuri na wanafunzi ukisisitiza masuala ambayo mifano hii inawakilisha, na kuwakumbusha wanafunzi madhumuni yake katika mazingira yao ya jumla ya kujifunzia.
1
U T U M E K A T I K A M I J I
3 Ukurasa wa 398 Mifano Halisi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online