Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 7 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Maombi ni muhimu kwa kila nyanja ya kujifunza, kukua, kutumia, na kuitikia kweli ya Mungu. Katika maombi, wewe na wanafunzi wako mna fursa ya kupata maagizo ya moja kwa moja na mwongozo wa Mungu kuhusu maana na matumizi ya masomo husika. Kwa hivyo, unapoingia katika wakati wa maombi pamoja na wanafunzi, kamwe usifikirie kuwa ni kitu ambacho lazima kifanywe kwa haraka, au kitu ambacho kinaweza kupuuzwa kabisa. Usichukulie kama jambo la kawaida sana au lisilo la lazima; mara zote waulize wanafunzi kama wana maombi yoyote maalum, kwamba yanahusiana na mawazo na kweli zinazowasilishwa katika somo au la. Onyesha kwa kielelezo chako na mtazamo wako kwamba maombi ni ya maana, ni njia ya ajabu ya vitendo na yenye manufaa katika kutumia kweli. Wakumbushe kwamba kwa kupeleka mahitaji yao mahususi kwa Mungu katika mwangaza wa kweli fulani mahususi, Bwana ataimarisha mawazo hayo maishani mwao, na kuwapa fursa maalum za kuyatumia katika huduma zao. Bila shaka, kila kitu kinategemea kiasi cha muda ulio nao katika kipindi chako, na jinsi ulivyoupangilia. Bado, maombi ni sehemu yenye nguvu na yenye uwezo wa kukutana na mafundisho yoyote ya kiroho, na kama unaweza, yanapaswa kuwa na nafasi yake kila wakati, hata ikiwa ni maombi mafupi ya muhtasari kwa ajili ya yale ambayo Mungu ametufundisha, na azimio la kuishi matokeo yake kama Roho Mtakatifu anavyotufundisha.
4 Ukurasa wa 401 Ushauri na Maombi
1
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online