Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 7 7

Uinjilisti na Vita ya Kiroho Kufungwa kwa Mtu Mwenye Nguvu

SOMO LA 2

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 2, Uinjilisti na Vita vya Kiroho: Vita vya Kiroho – Kumfunga Mtu Mwenye Nguvu . Lengo la jumla la somo hili ni kuwapa wanafunzi ufahamu ulio wazi wa maarifa na utendaji wa uinjilisti na vita vya kiroho katika mazingira ya mijini. Mkazo ni uinjilisti; msisitizo wa vita vya kiroho unaunganishwa na ukweli kwamba uinjilisti kimsingi ni ukombozi kutoka katika nguvu za Shetani na utawala wa dhambi na athari zake. Hili ni muhimu kutambua, hasa kwa sababu ya muda mfupi tulionao wa kuangazia masuala haya yenye umuhimu na upana kiasi hicho. Malengo haya yameelezwa kwa uwazi katika sehemu ya “Malengo ya Somo” na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote na wakati wa majadiliano na muda wote uwapo na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Tumia malengo kufundisha na kufanya mapitio ya maudhui ya somo lenyewe. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi cha darasa. Kadiri utakavyosisitiza zaidi malengo halisi ya somo, ndivyo itakavyokuwa bora zaidi kwa wanafunzi wako. Mkazo huu pia hukupa “kulabu” za vitendo ambazo unaweza “kutundikia” kweli, taarifa, na mawazo ambayo huja wakati wa majadiliano . Vuta usikivu wa wanafunzi kuelekea malengo haya, kwani, kiuhalisia, huu ndio moyo wa dhumuni lako la kielimu unapofundisha vipindi vya somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kulenga kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyasisitiza haya kila wakati, kuyakazia na kuyarudia tena na tena unapoendelea na somo. Ibada hii inakazia utayari wa Bwana Yesu kujinyenyekeza ili kuwa kama sisi. Huu ni ujumbe maarufu wa Maandiko Matakatifu (rej. Mt. 11:29; 20:26-28; Lk. 22:27; Yn. 13:14; Mdo. 10:38; Mdo 20:35; Rum. 14:15; 15:3-5; 1 Kor. 10:33; Ef. 5:2; 1 Pet. 2:21; 4:1; 1 Yoh. 2:6). Unyenyekevu wa Yesu ndiyo msingi wa huduma zote, utume, na kuwafikia wengine. Katika yote tuliyo nayo na tufanyayo, tunapaswa kuiga roho ya kujidhili ya Bwana wetu Yeshua ambaye alikuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya wengine. Yesu

 1 Ukurasa wa 405 Utangulizi wa Somo

2

U T U M E K A T I K A M I J I

 2 Ukurasa wa 405 Malengo ya Somo

 3 Ukurasa wa 405 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online