Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 8 1

Kwa namna yoyote utakayoamua kulitekeleza hili, imani yetu ya msingi zaidi ni kwamba uwezo wa kielimu sio kiwango cha uongozi wa Kikristo, bali wito, karama, na nguvu. Wasaidie wanafunzi wako, usiwakatishe tamaa kwa kazi hizi. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na usisitize kwamba jambo muhimu ni uelewa wao wa kile walichosoma, si weledi wao katika uandishi. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa namna inayoharibu juhudi za kuwatia moyo na kuwajenga. Pamoja na hayo, hatutaki pia kudunisha uwezo wao kwa namna yoyote. Tafuta namna ya kuweka uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo.

2

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online