Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 8 3
Mkazo kuhusu Uzazi Ukuaji wa Kanisa – Kuongezeka katika Idadi na Ubora
SOMO LA 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 3, Mkazo kwenye Uzazi: Ukuaji wa Kanisa - Kuongezeka katika Idadi na Ubora. Lengo la jumla la somo hili ni kuwapa wanafunzi wako uelewa wa uinjilisti, ufuasi, na upandaji makanisa katika muktadha wa jamii za mijini. Ikiwa wanaanthropolojia wa mijini wako sahihi, ndani ya miaka 20-25 ijayo, mtu mmoja kati ya kila watu watatu atakuwa mkazi wa mitaa duni ya mijini! Kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, watu wengi zaidi wanaishi mijini kuliko vijijini au maeneo ya kilimo; umisheni katika karne ya 21 lazima utakuwa ni kazi ya utume katika miji. Hoja ya somo hili ni kwamba njia ya haraka zaidi, yenye ufanisi zaidi, na yenye kuzaa matunda zaidi ya kiroho ni upandaji makanisa mijini kwa kuzingatia tamaduni tofauti tofauti. Jukumu lako katika somo hili ni kuwapa changamoto wanafunzi wako kujiandaa kwa ajili ya wimbi jipya la Huduma na Utume. Watahitajika kuwa sehemu ya kada ya watenda kazi wa mijini ambao, wakijitoa wenyewe kwa Mungu kwa kujidhili na uelekevu mpya, wanaweza kuathiri, hata kubadilisha maelfu ya jamii wanaposonga mbele katika utume, katika nguvu za Roho Mtakatifu, na ujumbe wa Kristo, kwa ajili ya utukufu wa Mungu Baba. Masomo haya yameundwa kwa uangalifu ili kuwatembeza wanafunzi wako katika mchakato wa upandaji makanisa katika jamii za mijini. Katika somo la kwanza, tunaanza mafunzo yetu na somo la Ukuaji wa Kanisa: Kuongezeka katika Idadi na Ubora. Hapa tunathibitisha dhana moja muhimu sana katika kuelewa umisheni katika jiji: Ubwana wa Yesu Kristo. Kama Bwana aliyefufuka na Masihi Mpakwa-Mafuta wa Mungu, Yesu ameinuliwa hadi mahali pa kuwa Kichwa juu ya vitu vyote, kwa Kanisa na ndiye Bwana wa mavuno. Katika somo la pili , Kupanda Makanisa ya Mijini : Upanzi tunatambulisha dhana muhimu ya oikos katika uinjilisti wa mijini. Hapa tunaonyesha jinsi oikos ilivyo mtandao wa uhusiano wa kindugu wa kawaida, urafiki, na vyama vinavyounda mtandao mkubwa wa mtu kijamii. Tutaanza na muhtasari wa oikos katika Agano Jipya, kisha tutachunguza maana ya wazo hili muhimu kwa uinjilisti katika tamaduni tofauti za mijini. Katika somo la tatu tunaeleza zaidi awamu kuu ya pili ya upandaji kanisa, Kuandaa , kupitia wazo la ufuatiliaji, au kuwaingiza wanafunzi wapya katika Kanisa. Tukisisitiza kwamba Kanisa ni njia ya Mungu ya kuwaleta Wakristo wapya katika ukomavu, tunatoa vipengele na vidokezo muhimu vya zoezi la kuwafuatilia waumini wapya katika Kristo.
1 Ukurasa wa 419 Utangulizi wa Somo
3
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online