Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Katika somo hili pia tutaangalia kwa karibu kazi ya kuwafuasa waumini wanaokua. Hatimaye, katika somo la nne tunazingatia jukumu letu katika kusaidia makanisa mapya kusonga mbele kuelekea uhuru kupitia Uwezeshaji, na awamu ya mwisho ya upandaji kanisa mijini: Mpito. Tutafafanua kusudi, mpango, na mitazamo inayohusiana na uwezeshaji kupitia vipengele vinne vya kibiblia vya uongozi wa kanisa la mijini. Bila shaka, uongozi wa kitumishi wa kimungu ni muhimu ili kuwa na kanisa linalokua katika jiji. Katika masomo haya yote itakuwa muhimu kwako kusisitiza na kuvuta umakini wa mwanafunzi kwenye malengo. Dhamiria tangu mwanzo kuyasisitiza katika somo lote, katika kila sehemu na nyanja, na hasa wakati wa majadiliano na muda wote wa kuwapo pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano kwamba wataelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyoongezeka. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi. Vuta umakini wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, katika maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyaangazia haya kila mara, ili kuyasisitiza na kuyakazia tena na tena kadri unavyoendelea. Ibada hii inazingatia umuhimu wa Agizo Kuu kwa Mitume, na jinsi walivyouchukulia wito huu kwa uzito, hata kuwa tayari kukabili mateso, kukataliwa, na kifo ili kuutimiza. Katika uhalisia, ibada hii iko kwenye Agizo Kuu lenyewe, na muhtasari mzuri kutoka kwa J. B. Green unaweza kuwa wa manufaa unapowaelekeza wanafunzi kwenye moyo wa umisheni wa Kikristo, ambao ni amri ya Yesu ya kwenda kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi. Kupitia Agizo Kuu la Mathayo 28:16-20 Yesu anawaelekeza wafuasi wake juu ya umuhimu endelevu wa uanafunzi kwa vizazi vyote... Yesu alitumia huduma yake katika dunia “kufanya wanafunzi” ndani ya Israeli (rej. Yn. 4:1), na aliwaagiza wanafunzi wake “kufanya

3

U T U M E K A T I K A M I J I

 2 Ukurasa wa 419 Malengo ya Somo

 3 Ukurasa wa 419 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online