Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 8 5
wanafunzi” katika mataifa (Mt. 28:16-20; taz Mataifa). Maana ya wazi ya “kufanya wanafunzi” ni kutangaza ujumbe wa Injili miongoni mwa wale ambao bado hawajapokea msamaha wa dhambi (Lk. 24:46-47; Yn. 20:21; taz. Msamaha wa Dhambi). Amri hiyo inapata utimilifu wa ajabu na dhahiri katika shughuli za Kanisa la kwanza (k.m., Mdo. 14:21), ambapo wanafunzi walitoka Yerusalemu hadi Yudea, hadi Samaria (taz. Wasamaria), hadi miisho ya dunia wakitangaza ujumbe wa Yesu na kufanya wanafunzi. Katika Kanisa la kwanza, kuamini ujumbe wa Injili kulimaanisha kuwa mfuasi (rej. Mdo. 4:32 na 6:2). Amri ya Utume Mkuu ilitolewa angalau kwa wanafunzi kumi na mmoja waliosalia (rej. Mt. 28:16), lakini katika jukumu lao wenyewe kama wanafunzi, wao ni kielelezo kwa wanafunzi wote. Yesu anapozungumza na wanafunzi wake na kuwaamuru ‘wafanye wanafunzi kutoka katika mataifa yote,’Yesu anawaambia waendelee na kazi aliyoanza nao. Wito huu kwa walioitiwa Mitume wa kwanza vile vile ni wito wa wazi wa Bwana kwa kizazi kizima cha Wakristo katika enzi hii kwenda hadi miisho ya dunia na kushuhudia kwa kila watu habari njema ya Injili. Mitume wanafunua katika kifungu hiki ahadi yao isiyobadilika ya kuwa waaminifu kwa Agizo, bila kujali upinzani wala gharama yoyote ambayo inapaswa kulipwa. Hapa ndipo utume na huduma ya mijini inapoanzia: upatikanaji usio na masharti ili kufanya mapenzi ya Kristo, kwa namna yoyote. ~ J. B. Green. Dictionary of Jesus and the Gospels. (toleo tepe) Downers Grove, IL: InterVarsity, 1997. uk. 188. Zingatia kwa uangalifu sehemu za Kujenga Daraja katika masomo haya. Sehemu hizi zimeundwa mahususi ili “kuchochea pampu za kiakili na kiroho” za wanafunzi wako, ili kuwaweka tayari kuzingatia maudhui ya kibiblia ya somo, na matokeo yanazohusiana na maudhui hayo. Kuwa mwangalifu kuhakikisha kwamba unaongoza wakati wako vizuri katika matumizi yako ya taarifa ya kipengele cha Kujenga Daraja; ingawa matukio na mawazo yanayoshughulikiwa ni ya kuvutia, yanaweza kuchukua kiasi kikubwa cha muda wako wa somo, kutegemeana na jinsi ulivyotenga muda wako kwa somo husika.
3
U T U M E K A T I K A M I J I
4 Ukurasa wa 421 Kujenga Daraja
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online