Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 8 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Sehemu hii inaangazia kweli za msingi zilizoandikwa kwa njia ya sentensi ambazo wanafunzi walipaswa kuwa wamepokea kutoka kwenye somo hili, yaani, kutoka katika video na mazungumzo yako pamoja nao. Kusudi lako linapaswa kuwa kuwasaidia wanafunzi wako kuelewa kanuni muhimu zilizo katika muundo wa methali, katika kauli rahisi, ya wazi ambayo inawawezesha kufanya muhtasari wa maarifa ya somo na kuwafundisha wengine. Kusudi la somo ni kufikia “vidokezo,” zile kanuni muhimu za ukweli ambazo wanaweza kutathmini, kutumia, na kushirikisha wengine katika maisha na huduma zao. Kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kweli za msingi ambazo zinapatikana katika somo kamwe si kupoteza muda. Mara nyingi, uwezo wetu wa kuwasaidia wanafunzi wetu kujishughulisha na dhana hizi utaamua kama wanaweza kutumia kweli hizi baadaye au la, katika kujijenga kibinafsi, kufundisha na kuhubiri kwao, na kuwafunza wengine. Kwa hiyo, hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa kwa uwazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwa sababu kazi yao ya jaribio na mitihani itachukuliwa kutoka kwenye vitu hivi moja kwa moja. Wakati sehemu ya kwanza ya somo inazingatia hitaji la wanafunzi kufahamu vema dhana zilizomo katika somo , kuanzia wakati huu lengo ni kuwasaidia wanafunzi wako kufahamu matumizi ya maarifa ya somo katika maisha yao binafsi . Kwa maneno mengine, wanafunzi wanahitaji angalau njia mbili za kutafakari wanapopitia somo. Njia ya kwanza ni ya kiakili na ya mazungumzo, na inalenga uwezo wao wa kushughulika na dhana ngumu ili kupata uelewa wa kile ambacho Maandiko yanafundisha hasa juu ya somo fulani. Njia hii ni muhimu. Hata hivyo, kuna njia nyingine, yenye umuhimu sawa na ya kwanza, ila yenye msisitizo tofauti kabisa. Njia hii ya pili ni ya kibinafsi na ya kiroho, na inalenga katika uwezo wao wa kutathmini maana ya kweli ambazo wamejifunza na zinavyohusiana na utendaji wao katika maisha na huduma. Njia hii kimsingi ni ya ubunifu . Kwa kuzingatia mawazo haya, mara zote itakuwa muhimu wakati fulani katika somo kubadili gia, na kuwawezesha wanafunzi kuanza kufikiria kupitia hali zao wenyewe kwa umakini na uhuru mkubwa. Maswali katika sehemu hii mara zote yameundwa kuwa “mshumaa” ili kuchochea moto wao katika kutafuta kujua zaidi. Kilicho muhimu hapa si kwamba wajibu maswali mahususi yaliyoandikwa

 5 Ukurasa wa 437 Muhtasari wa Dhana Muhimu

3

U T U M E K A T I K A M I J I

 6 Ukurasa wa 438

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online