Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 8 7

hapa chini, bali kwamba waweze kushughulika na dhana husika kwa namna ambayo wataelekeza mawazo yao kwenye tathmini na utendeaji kazi wa masuala na mada katika maisha na huduma zao wenyewe. Katika mazungumzo na wanafunzi wako, zingatia kutatua kada ya masuala kadha wa kadha, mashaka, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, kisha husianisha hayo na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichochezi tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au uje na maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali waliyo nayo. Mifano halisi hufanya kazi kwa kiasi fulani kama sehemu za “Kujenga Daraja” hapo juu, huku zikiwa na tofauti moja ya msingi. Wakati ambapo sehemu ya Kujenga Daraja ilikusudiwa ili kusaidia kutambulisha kwa wanafunzi wako mawazo na masuala yanayoshughulikiwa katika somo, Mifano halisi kimsingi ni matukio halisi au ya kufikirika yenye kusudi la kuwasaidia wanafunzi wako kuonyesha kwamba wanaweza kutumia kweli za somo katika muktadha wa hali halisi au inayoweza kutokea katika maisha. Mara nyingi inatokana na hadithi za kweli, na wakati wote inaakisi utata na ugumu wa kuhudumu katika jamii za mijini. Sehemu kubwa ya sehemu ya mifano halisi inahusisha uwezo wako wa kuwasaidia wanafunzi kuwa na hekima katika matumizi yao ya kweli katika mazingira au suala fulani mahususi . Ni imani yetu kwamba wanafunzi wako wataweza kutumia hekima ya kibiblia katika masomo haya. Kwa ujumla, njia tatu zifuatazo zitaweza kusaidia katika hili: 1. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kweli za hali au suala husika.

3

U T U M E K A T I K A M I J I

 7 Ukurasa wa 439 Mifano Halisi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online