Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 8 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
2. Baada ya kweli kuwa wazi, wasaidie wanafunzi wako kuamua ni maarifa na kanuni gani zinazohitajika kutumika kwa hali hiyo, na ni majibu mangapi yanaweza kuwa sahihi kuhusiana na suala hilo. 3. Watake wachague masuluhisho ya suala husika, au mbinu ambazo wangetumia, kutokana na utambuzi wa hali hiyo na kanuni za kibiblia zinazohitaji kutumika. Tafakuri ya aina hii inaweza kuwasaidia wanafunzi wako kutoka kwenye kuzingatia tu kweli, hadi kufikia kutumia kweli hizo za msingi zaidi katika maisha yao wenyewe na katika hali za maisha ya wengine. Sehemu hii tena inakupa fursa ya “kurundika” kweli kwa mara ya mwisho katika mioyo na akili za wanafunzi kabla ya kumaliza somo. Usije ukafikiri kwamba mbinu ya aina hii ni ya kupita kiasi, zingatia Maandiko yafuatayo: Flp. 3:1 – Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi 2 Pet. 1:12-15 – Kwa hiyo nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo. 13 Nami naona ni haki, maadamu nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha. 14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha. 15 Walakini nitajitahidi, kwamba kila wakati baada ya kufariki kwangu mpate kuyakumbuka mambo hayo. 2 Pet. 3:1 – Wapenzi, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika zote mbili naziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha. 2 Tim. 1:6 – Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Huduma ya “kukumbusha” ni mojawapo ya huduma muhimu ambazo mwalimu mcha Mungu anaweza kufanya. Usisite kusisitiza kweli za msingi kila wakati. Ni muhimu ukahakikisha kwamba wanafunzi wanazifanya kweli hizi kuwa zao.
3
8 Ukurasa wa 441 Mapitio ya Tasnifu ya Somo
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online