Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 8 9

Kusudia kuzifanya nyakati zako za kujifunza pamoja na wanafunzi kuwa fursa ya kuhuishwa na kuamka kiroho kama vile ulivyo wakati wa kutafakari na mazungumzo juu ya kweli . Ikiwezekana, panga wakati wako kwa njia ambayo unaweza kuruhusu maombi kwa ajili ya wanafunzi, na uhamasishe jambo hilo hilo katika maisha yao. Maombi yana uwezo mkubwa wa kuingiliana na mafundisho yako na kuzaa matunda maishani mwao kwa matokeo yenye nguvu. Bwana yuko tayari kuwasaidia wakue na kuwa zaidi kama Mwana wake, na kuwa na matokeo kadiri wanavyohitaji wanapojifunza na kutumia kweli hizi. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kazi ya wiki ijayo, hasa ile ya kuandika . Hii sio ngumu; lengo ni kwamba wasome maeneo waliyoagizwa vizuri kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile wanachodhani kimemaanishwa. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na usisitize kwamba jambo muhimu ni uelewa wao wa kile walichosoma, si weledi wao katika uandishi. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa namna inayoharibu juhudi za kuwatia moyo na kuwajenga. Pamoja na hayo, hatutaki pia kudunisha uwezo wao kwa namna yoyote. Tafuta namna ya kuweka uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo. Ubora unapaswa kutarajiwa kutoka kwa wanafunzi wako, na bila shaka, tunajua kwamba wanafunzi watakuwa na uwezo tofauti wa kufanya kazi za kiakili – kusoma, kuandika, na kadhalika. Ingawa tunataka kusisitiza utendaji bora wa kitaaluma, hatutaki kuinua viashiria hivi zaidi kuliko ulaini wa moyo, utayari wa kutii Neno la Mungu, na upatikanaji katika kumtumikia Kristo kama anavyowaongoza kwa Roho wake. Fuatilia kila wakati msisitizo wako juu ya maksi, kazi na utendaji wa kitaaluma. Haya ni muhimu , lakini sio muhimu kuliko yote. Zingatia jambo kuu: kupatikana bila masharti kwa ajili ya Kristo ili kumtii katika maisha yetu jinsi anavyotuelekeza.

 9 Ukurasa wa 442 Ushauri na Maombi

 10 Ukurasa wa 443 Kazi

3

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online