Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 9 1
Kutenda Haki na Kupenda Rehema Haki na Ishuke – Maono na Theolojia ya Ufalme Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 4, Kutenda Haki na Kupenda Rehema: Haki na Ishuke – Maono na Theolojia ya Ufalme . Lengo la jumla la somo hili ni kukupa msingi wa kimisheni, kitheolojia, na wa kimkakati kwa huduma hii muhimu katika maisha ya kiongozi wa Kikristo wa mjini. Tunakabiliana na masuala ya jamii ambazo kihistoria zimekuwa zikikabiliwa na msururu wa matatizo sugu ya kijamii, ukandamizaji wa kiroho, unyonyaji wa kiuchumi, na ukiukwaji wa kimaadili. Kuwa kiongozi wa Kikristo wa mjini ni sawa na kuwa mjumbe wa haki, rehema na amani ya Yesu Kristo, na kanisa analotumikia ni kituo na ubalozi halisi wa Ufalme wa Mungu, utawala unaotambulika kwa haki na huruma. Ili kufaidika na somo hili, ni lazima uyakubali maono haya kama yako, yaani, ni lazima uone kwamba kipengele muhimu katika uelewa wako na matumizi ya maarifa haya ni uwezo wako wa kujiona kama kiongozi wa haki na amani, na kanisa ambamo unamwabudu na kumtumikia Kristo kama kitovu cha haki na huruma hiyo. Pasipo kukubali kwako mwenyewe shauku hii katika maisha yako kama mkufunzi, utazuiwa kwa kiwango kikubwa katika uwezo wako wa kuwasaidia wanafunzi wako kukumbatia hili kama maono yao wenyewe. Unapojadili dhana mbalimbali, maswali, na masuala yanayotokana na yaliyomo katika somo hili, itakuwa muhimu kwako kuwa na ufahamu wa namna mada hii ya kudhihirisha haki na rehema katika upendo ilivyo hakika. Kwa njia nyingi somo hili lote ni jaribio la kuelewa na kudhihirisha maonyo rahisi lakini yenye nguvu ya Mika 6:6-8, uchambuzi na agizo ambalo linatoa muhtasari wa kile ambacho Mungu angetaka mtu na watu wake wawe na kufanya. Mik. 6:6-8 – Nimkaribie Bwana na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? 7Je! Bwana atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? 8Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako! Andiko hili ni muhtasari wa hukumu kuhusu aina ya huduma na ibada ambayo Bwana anatamani na kudai. Kwa upande mmoja, Mungu hapendezwi na utii wa kiibada, kwa namna ya nje, ya
SOMO LA 4
1 Ukurasa wa 445 Utangulizi wa Somo
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online