Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 9 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

kidesturi na isiyo na uhai ndani yake. Badala yake, Mungu anataka udhihirisho wa nje wa shauku ya ndani kuhusu mapenzi yake na namna yanavyotimizwa katika uhusiano wetu na Yeye na uhusiano wetu na wengine. Mungu anawataka watu wake watende kwa haki. Hii maana yake, waonyeshe haki na uadilifu katika shughuli zao zote na wengine, kwamba wapende rehema, wakionyesha kujali na huruma ya kweli katika nyanja zote za uhusiano wao na wengine, na hatimaye, waishi kwa unyenyekevu na Mungu wao, wakihusiana na Mungu kwa mioyo ya shukrani na unyenyekevu unaojengwa juu ya agano lake la neema na utunzaji wake. Haya ndiyo ambayo, katika Maandiko yote, Mungu ameonyesha wazi kuwa anatamani. Kwa hivyo madai ya maandiko yafuatayo hapa chini sio ya riwaya au haba: Kumb. 10:12-13 – Na sasa, Israeli, Bwana, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche Bwana, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; 13 kuzishika amri za Bwana na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri? 1 Sam. 15:22 – Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Mit. 21:3 – Kutenda haki na hukumu Humpendeza Bwana kuliko kutoa sadaka. Isa. 1:16-19 – Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; 17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. 18 Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. 19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi. Isa. 58:6-11 – Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira? 7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online