Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 9 3

usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? 8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde. 9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu; 10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. 11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. Kufanya haki na kupenda rehema ndiyo njia ya hakika zaidi tunayoweza kutoa ibada inayokubalika kwa Mungu, na kuthibitisha kwa hakika kwamba tunatembea kwa unyenyekevu pamoja naye. Kwa bahati mbaya, historia ya viongozi wa Mungu na watu wake mara nyingi imejaa matendo ya udhalimu (taz. Mik. 2:1-2; 3:1-3; 6:11), kuwa wabinafsi na wasio waaminifu kwa jirani zetu (Mik. 2:8-9; 3:10-11 6:12), na kutembea kwa majivuno na kiburi mbele za Mungu (2:3). Lengo letu katika somo hili ni kuwajenga wanafunzi katika theolojia ya kweli hizi, na kuchunguza matokeo yake kwa wale wanaoishi mjini. Malengo ya somo hili ni yenye nguvu na muhimu, kwa hivyo tafadhali yazingatie kwa uangalifu. Yameelezwa kwa uwazi, yameunganishwa kwa uangalifu katika somo lote, na yameundwa kwa ajili ya wewe kuyasisitiza kadri unavyoendelea na somo, hasa wakati wa majadiliano na muda wote uwapo pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo uwezekano wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya unavyoongezeka. Malengo yaliyo hapo juu yameundwa ili kuweka mwelekeo wa mchakato mzima wa kujifunza somo hili. Falsafa yako lazima iwe ya kuunganisha mawazo, shughuli, na masuala yote mbalimbali yanayoangaziwa katika somo hili. Yanawakilisha, kwa hakika, kile tunachotumaini kwamba wanafunzi watahifadhi, kuelewa, kukariri, na kukumbatia kama matokeo ya kushughulika na maarifa yaliyomo

4

U T U M E K A T I K A M I J I

 2 Ukurasa wa 445 Malengo ya Somo

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online