Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

1 9 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

katika somo hili. Ni ya muhimu kwa yote unayofanya, na yanapaswa kurejelewa mara kwa mara na kujadiliwa wakati wote. Kwa sababu hiyo, usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi. Vuta umakini wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, katika maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyaangazia haya kila mara, ili kuyasisitiza na kuyakazia tena na tena kadri unavyoendelea. Ibada hii kimsingi inalenga kwenye amri ya pili, Law. 19:18 “Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.” Kuishi na kupata uzoefu wa mahusiano yanayokua katika ukaribu na Mungu kutatudai tutende haki na kupenda rehema, na kuionyesha katika maisha ya wale tunaokutana nao. Tunadhihirisha upendo huu wa jirani, haki hii na rehema katika muktadha wa matendo maalum, mahususi, na thabiti ya upendo na huruma kwa kaka na dada zetu, majirani zetu, na hata adui zetu. Wazo la kuwa mlinzi wa ndugu yetu ndicho kiini cha maana ya kuwa na uhusiano wa kweli na Mungu. Kumpuuza ndugu (jirani) ni kunaswa katika utando wa wivu, udhaifu, na ukatili wa Kaini, ambaye kwa mujibu wa maelezo ya Yohana juu ya kisa hicho alimuua ndugu yake Habili kwa sababu matendo yake mwenyewe yalikuwa maovu na matendo ya ndugu yake yalikuwa ya haki, 1 Yohana 3:11-15. Kukubali maono haya ya mahusiano ya kibinadamu kama moyo wa ufahamu wote wa kweli wa Mungu ndiyo namna ya kuelewa kile ambacho Yohana anarudia mara kwa mara juu ya haja ya kuthibitisha na kuonyesha upendo wa mtu kwa Mungu kwa njia ya upendo kwa wengine (taz. 1 Yoh. 4:7-21; Yn. 13:34-35; 15:12). Unapojadili ukweli wa hadithi ya Mwanzo na wanafunzi wako, tafuta kuwasaidia kuelewa uwiano wa hadithi hii ya kale na ukosefu wa haki na ukatili unaofanyika katika jamii nyingi za mijini leo. Njia yetu pekee ya kutoka katika ukungu huu wa ukatili ni kugundua tena tabia hii ya msingi ya mtu anayemjali Mungu kweli: kuwa mlinzi wa jirani yetu na ndugu yetu. Katika upambanuzi wowote wa kiroho ulio wa kweli, huu ndio utambuzi wa msingi kuhusiana

 3 Ukurasa wa 445 Ibada

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online