Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 9 5
na kuishi maisha yetu kama viongozi ambao tunatenda haki na kuonyesha huruma ya Mungu.
Sehemu za Kujenga Daraja katika somo hili ziliundwa ili kuwawezesha wanafunzi wako kujiandaa kwa ajili ya kazi ngumu ya kiakili ya kuzingatia maono na theolojia ambayo ni msingi wa mamlaka ya Mungu ya kudhihirisha haki na huruma katika maisha yetu na kupitia makanisa yetu. Ili kuchunguza maudhui ya kitheolojia zinazohusika na hili, utahitaji kuwasaidia wanafunzi wako kuyatafakari kimakusudi mawazo ambayo kwa kawaida huwa wanayachukulia kuwa ya kawaida au hawayatafakari kwa uangalifu mara nyingi. Tumia maswali na mawazo haya ili kuwachochea wanafunzi wako kuibua usikivu na shauku zao juu ya maswali yao ya msingi kuhusiana na kuwapenda wengine, kupendwa, na kumpenda Mungu, na jinsi upendo huu unavyohusiana, pamoja na masuala na matokeo ya kushindwa kudhihirisha haki hii na huruma kwa wengine. Dhana ya Imago Dei Unapochunguza maana za imago Dei pamoja na wanafunzi wako, linaweza kuwa jambo la msaada kwako kusoma muhtasari mzuri na mfupi wa maana zake kuu katika Maandiko kutoka kwa profesa Ryken kuhusu jambo hili muhimu: Zaburi ya 8 ni usemi bora wa kulinganisha baina ya Mungu na watu. Katika mstari wa 4 swali la mtunga-zaburi kwa Mungu, “Mtu ni kitu gani” lilitokana na kutafakari kwake juu ya kweli tatu ambazo ni uumbaji wa vitu visivyo na uhai, ubinadamu na uungu. Sababu ya kwa nini mtunga-zaburi angeweza hata kuuliza swali hili ni kwamba wanadamu ni wabeba sura ya Mungu (Mwa. 1:26-27) na wanajitambua. Kwa sababu ya imago Dei (“sura ya Mungu”), ulinganisho ufuatao unaweza kutambuliwa katika Maandiko. Kiini cha imago Dei ni haiba. Mungu na wanadamu wanaweza kuwasiliana kiakili (Zab. 8; Isa. 6:8-13). Wote wanaweza kupokea taarifa (Mwa. 1:28-30; Ebr. 1:1-2), kuwaza mawazo (Mwa. 2:19; 2:23) na kuchakata taarifa (Isa. 1:18-20). Ijapokuwa ujuzi wa Mungu hauna kikomo katika usahihi na yaliyomo ndani yake (Rum. 11:33-34; Mt.
4 Ukurasa wa 449 Kujenga Daraja
4
5 Ukurasa wa 450 Muhtasari
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online