Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 9 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
11:21-24), ujuzi wa mwanadamu haujakamilika (1 Kor. 2:9; 13:12) katika ubora wake na ni potofu katika ubaya wake (Efe. 4:17-18). Hali ya kihisia ya Mungu (Mwa 6:6; Mt 25:21; 2 Kor 7:6) mara zote ipo katika uwiano mkamilifu na haitegemei mtu yeyote nje ya Uungu wa Utatu kwa habari ya ukamilifu wake (Hos. 11:8-9; Mdo 17:25; Yn. 17:24-26). Mungu ndiye mpenzi asiyeacha kupenda (Yer. 31:3; Hos. 11:1-9). Ingawa wanadamu wanaweza kuonyesha hisia nzuri (Zab. 13:5-6; Mk. 12:20-30; 2 Kor. 1:24-2.4; 2 Yoh. 4), upendo wao mara nyingi hupungua (Ufu. 2:4), unaelekezwa katika kupenda uovu (2 Tim. 3:2, 4) na hufurahi katika jambo lisilofaa (Zab. 13:4; Mik. 3.2; 1 Kor. 13:6). Pia wanajitoa wenyewe kwa “tamaa za kudhalilisha” (Rum. 1:26). Chaguzi za Mungu daima ni za hekima na za haki (Mwa. 18:25; Isa. 10:13; Rum. 16:27), ambapo uchaguzi wa kibinadamu mara nyingi ni upotovu (Rum. 1:32). Ingawa kuna mwingiliano fulani katika yafuatayo, ulinganisho unaonekana pia katika maeneo kama tabia (Isa. 54:5; Hos. 3:1-3; Yer. 5:7, 8; 1 Pet. 1:14, 15), lugha za picha/mifano (Yoh. 1:19; Isa. 1:6, 7; Luke 3:22; Mt. 10:16), mahusiano ya kifamilia (Yer. 5:7, 8; 31:32; Efe. 5:28; Ufu.21:2) na taswira za kazi (Zab. 23; Zek. 11:17; Mt. 13:55; Yn. 10:11; 1 Kor. 3:5-17; Ebr. 11:10; 1 Pet. 5:2). Ingawa wakati na nafasi vinawafunga wabeba sura ya Mungu (Zab. 90:9-10; 139:7-9) wanashiriki mwendelezo fulani wenye kikomo na Mungu wa milele (Zab. 90:2) asiye na mipaka (Zab. 139:7-9), asiyetegemezi (Mdo. 17:25), sikuzote wao watakuwa viumbe tegemezi (Mwa. 1:27; Zab. 100:3) wanao wahitaji wanadamu wengine (Mwa. 2:18), taarifa za kiungu (Mt. 4:4; 1 Kor. 2:6-9) na Mungu mwenyewe (Yoh. 15:5, 11; 17:3; 16:5-11; 1Kor. 6:17).
4
U T U M E K A T I K A M I J I
~ Leland Ryken. Dictionary of Biblical Imagery . (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 336-337.
Sehemu ya Muhtasari wa Dhana Muhimu inakuruhusu kuwa na uchanganuzi wa haraka wa mawazo makuu, mafundisho, na kweli kuu zilizoshughulikiwa katika somo. Dhana hizi zinawakilisha kweli za msingi za vipindi vyote vya mafunzo, zilizoandikwa katika muundo wa sentensi rahisi. Mawazo haya yanakusudiwa kuwa jumbe za kuzingatia za somo, yaani, maarifa ambayo uwasilishaji, mijadala, na uchunguzi wa somo ulikusudiwa kuyaibua na kuyaweka wazi kwa wanafunzi. Kujizoeza kauli hizi ndiyo namna
6 Ukurasa wa 464 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online