Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 1 9 7

yako ya kusisitiza mawazo makuu ya vipindi vya masomo katika akili za wanafunzi, na kuwapa marejeleo yaliyokusanywa kama muhtasari wa somo. Hakikisha kuwa dhana hizi zimefafanuliwa wazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwa sababu kazi yao ya majaribio na mitihani itachukuliwa kutoka kwenye vitu hivi moja kwa moja. Sehemu ya Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi inampa mwanafunzi changamoto ya kutendea kazi matokeo ya somo katika maisha na huduma yake. Ni rahisi sana kwa wanafunzi kusahau kwamba lengo la kazi yetu si kuzingatia mawazo tu, bali kuunganisha maudhui ya somo na Sitz im Leben yao halisi (kwa Kijerumani “hali katika maisha”). Kila mwanafunzi lazima apewe changamoto ya kutafakari umuhimu binafsi wa kweli zilizomo katika somo kwa maisha yake mwenyewe, na kuchunguza mawazo hayo kadiri yanavyoweza kuhusiana na huduma yake. Kwa hivyo, jukumu lako ni kuwawezesha wanafunzi wako kufikiria kupitia kweli kuu huku jicho moja likielekea hali zao wenyewe. Unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini ili kuchochea shauku zao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, lakini ni kwako wewe, katika mazungumzo na wanafunzi wako, kutatua kada ya masuala kadha wa kadha, mashaka, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wao, kisha husianisha hayo na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwa ajili swali fulani lililotokana na video, au jambo maalum ambalo linafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vichochezi tu, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chagua na uchukue kutoka katika hayo, au uje na maswali yako mwenyewe. Jambo la muhimu ni tija ya maswali hayo sasa, kwa muktadha wao na kwa maswali waliyo nayo.

 7 Ukurasa wa 465

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi

4

U T U M E K A T I K A M I J I

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online