Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
1 9 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mafanikio ya jumla ya wanafunzi katika mazingira ya kujifunza katika kundi ni wao kujifunza kadiri wanavyosoma kibinafsi, na vile vile wanapokusanyika na wanafunzi wenzao katika mazungumzo, majadiliano, na maombi. Yote mawili, yaani kujifunza kwa mtu binafsi na katika kikundi ni muhimu. Ili kufikia mafanikio na ufanisi katika muda wa kujifunza, hakikisha unasisitiza kuhusu umuhimu wa kuwa na maandalizi binafsi na ya kikundi. Utahitaji kuhakikisha kwamba unawakumbusha na kuwapa changamoto wanafunzi wako kutenga muda bora wa kukamilisha kazi yao kwa ajili ya somo lijalo, na kuwakumbusha kuzingatia hasa usomaji wa maeneo waliyoagizwa, na kazi za uandishi wa muhtasari wa usomaji wao. Hii sio ngumu; lengo ni kwamba wasome maeneo waliyoagizwa vizuri kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile wanachodhani kimemaanishwa. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na usisitize kwamba jambo muhimu ni uelewa wao wa kile walichosoma, si weledi wao katika uandishi. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa namna inayoharibu juhudi za kuwatia moyo na kuwajenga. Pamoja na hayo, hatutaki pia kudunisha uwezo wao kwa namna yoyote. Tafuta namna ya kuweka uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo.
8 Ukurasa wa 471 Kazi
4
U T U M E K A T I K A M I J I
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online