Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 5 5
Kufundisha Sehemu ya II na ya III: Mtaala wa Cornerstone
• Kwanza, soma kwa umakini Utangulizi unaopatikana kwenye uk. 9, na upitie Kitabu cha Mwanafunzi na Mwongozo wa Mkufunzi ili kupata uelewa wa maudhui ambayo yatazungumziwa. Kitabu cha Mwanafunzi kina masomo na kazi zote, pamoja na marejeleo (yaliyoonyeshwa kwa ishara katika pambizo: &) kwa Vidokezo vya ziada vya Mshauri ambavyo vinaweza kupatikana katika toleo hili. Kila dokezo linarejelewa na nambari za ukurasa kukusaidia kurudi nyuma na kwenda mbele kati ya Kitabu cha Mwanafunzi na Mwongozo wa Mkufunzi. Mitihani ya kifungu na Jedwali la Majibu vinaweza kupatikana kwenye dashibodi ya WIU. • Pili, unahimizwa sana kutazama mafundisho yaliyo katika video zote mbili kabla ya kuanza kwa kozi. • Tatu, unapaswa kusoma nyenzo zote ulizopewa zinazohusiana na mtaala, iwe ni vitabu vya kiada, makala au viambatanisho. • Nne, inaweza kuwa na manufaa kupitia mada muhimu za kitheolojia zinazohusiana na kozi kwa kutumia kamusi za Biblia, kamusi za kitheolojia, na vitabu vya mafafanuzi ili kuhuisha ujuzi wako wa mada kuu zinazozungumziwa katika mtaala. • Tano, tafadhali fahamu kwamba wanafunzi hawapimwi kwenye kazi za usomaji . Hizi zimetolewa ili kuwasaidia wanafunzi kupata ufahamu kamili wa kile ambacho somo linafundisha, lakini si lazima wanafunzi wako wawe wasomaji bora ili kuelewa kile kinachofundishwa. Kwa wale ambao mnapokea mtaala huu katika tafsiri yoyote tofauti na Kiingereza, nyenzo zinazotakiwa kwa ajili ya usomaji zinaweza zisipatikane katika lugha yako. Tafadhali chagua kitabu kimoja au viwili vinavyopatikana katika lugha yako – kimoja ambacho unadhani kinawakilisha vyema kile kinachofundishwa katika mtaala huu – na badala yake uwape wanafunzi wako hicho. • Hatimaye, anza kufikiria kuhusu maswali muhimu na maeneo ya mafunzo ya huduma kwa vitendo ambayo ungependa kuangazia pamoja na wanafunzi kwa kuzingatia maudhui ya kozi.
Kabla ya Kozi Kuanza
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online