Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
5 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kabla ya kila somo, unapaswa kutazama tena maudhui ya kufundishia ambayo yanapatikana katika video ambayo ni mahususi kwa kipindi hicho cha darasa, na kisha uunde sehemu ya Kujenga Daraja na ya Uhusianishaji kwa ajili ya somo hili.
Kabla ya Kila Somo
Pitia upya Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na ukusanye mawazo kwa ajili ya shughuli za kujenga Daraja zinazowezekana (njia mbili mpaka tatu za kujenga Daraja zinatolewa ambazo unaweza kutumia, lakini uwe huru kujitengenezea za kwako, kama utaona hilo litakusaidia zaidi.) Kisha, tengeneza sehemu ya kujenga Daraja ambayo inawapeleka wanafunzi kwenye maudhui ya somo na kukamata usikivu wao. Kama ilivyo kanuni, njia za kujenga Daraja zinaangukia katika makundi matatu. Vinasa usikivu , zinakamata usikivu wa wanafunzi na kuwapeleka kwenye mada ya somo. Vinasa usikivu, vinaweza kutumiwa vyenyewe katika darasa lenye wanafunzi wenye hasama nzuri au pia vinaweza kuchanganywa na mbinu nyingine kama ambavyo imeelezwa hapa chini. Mifano: • Kuimba uwimbo wa ufunguzi unaohusiana na ujumbe wa somo. • Kuonyesha katuni au kichekesho fulani ambacho kinahusiana na suala linalozungumziwa katika somo. • Kuwaomba wanafunzi wasimame upande wa kushoto wa chumba cha darasa kama wanaamini kwamba ni rahisi kuwafundisha watu namna ya kupata wokovu kwa kutumia vitabu vya Injili na kisha uwaambie wengine wanaoamini kwamba ni rahisi kuwafundisha watu namna ya kupata wokovu kwa kutumia vitabu vya Nyaraka wasimame upande wa kulia. Mbinu za kusimulia hadithi hapa anaweza kuwa mkufunzi ndiye anayesimulia hadithi ambayo inaonyesha umuhimu wa kile kinachoenda kufundishwa katika somo au anaweza kuwaambia wanafunzi wasimuliane yale waliyopitia kuhusiana na mada inayoenda kujadiliwa. Mifano:
Kuandaa Sehemu ya Kujenga Daraja
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online