Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 5 7

• Katika somo la kazi za mchungaji, Mkufunzi anaweza kuhadithia hadithi kuhusiana na namna ya kufanya mazishi na akawaambia maswali na changamoto ambazo zilionekana katika tukio hilo. • Katika somo kuhusu uinjilisti, mkufunzi anaweza kuwaomba wanafunzi waseme yale waliyowahi kukutana nayo wanaposambaza Injili. Shughuli zenye kuibua matatizo huibua maswali yenye changamoto ili yajibiwe na wanafunzi na kuwaongoza katika maudhui ya somo kama chanzo cha kujibu maswali hayo, au unaweza kuwaelekeza wanafunzi kuyaandika maswali ambayo bado hayajajibiwa kuhusiana na mada itakayojadiliwa. Mifano: • Kuwasilisha mifano kutoka katika hali halisi za huduma ambazo zinahitaji maamuzi ya kiuongozi na uwaruhusu wanafunzi wajadili ni hatua gani ingekuwa sahihi kwa hali husika. • Maswali yaliyotengenezwa kama: “unapohubiri kwanye mazishi ni muhimu zaidi kwa muhubiri kuwa mkweli au kuwa na huruma? Eleza kwanini?” Haijalishi njia inayotumika, msingi wa kufanikisha sehemu ya Kujenga Daraja ni kuhakikisha unajenga Daraja linalo waingiza wanafunzi katika maudhui ya somo. Unapopanga sehemu ya Kujenga Daraja, wakufunzi wanatakiwa kuandika kauli ya mpito ili kutengeneza daraja kutoka kwenye mbinu hii ya kulitambulisha somo mpaka kwenye maudhui ya somo. Kwa mfano kama maudhui ya somo yalikuwa kuhusu ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni nafsi iliyo sawa na nyingine katika ukamilifu wa Mungu, shughuli ya Kujenga Daraja inaweza kuwa kuwafanya wanafunzi wachore haraka ishara inayomwakilisha vyema zaidi Roho Mtakatifu kwao. Baada ya wao kuonyesha michoro yao na kueleza kwanini wameichora ile, mkufunzi anaweza kuweka kauli ya mpito kama ambavyo inaonekana katika mistari inayofuata: Kwa sababu Roho Mtakatifu mara nyingi anawakilishwa na alama kama moto au mafuta katika Maandiko kuliko kuonyeshwa kama sura ya kibinadamu kama ilivyo kwa Baba au Mwana, imekuwa ngumu wakati fulani kuwasaidia watu kuelewa kwamba Roho

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online