Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

5 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Mtakatifu ni nafsi kamili na ni Mungu anayefikiri, anayetenda, na kuongea yeye kama yeye kama tu ilivyo kwa Mungu Baba au Yesu Kristo. Katika somo hili tunataka tuweke msingi wa kimaandiko kwa ajili ya kuelewa kwamba Roho ni zaidi ya ishara tu ya “nguvu ya Mungu” Na fikiria kuhusu njia ambazo tunaweza kuzitumia ili kuliweka hili wazi kwa watu katika makusanyiko yetu. Hii ni kauli ya mpito yenye manufaa sana kwa kuwa inawaongoza wanafunzi katika kile ambacho wanatakiwa wakitarajie kutoka kwenye maudhui ya somo na pia inawaandaa kwa baadhi ya vitu ambavyo vitajadiliwa katika sehemu ya Uhusianishaji ambayo inakuja baadae, japokuwa unaweza kutengeneza kauli yako ya mpito kulingana na majibu ya wanafunzi wakati wa sehemu ya Kujenga Daraja. Ni muhimu wakati wa kupanga ufikirie pia nini kitakachosemwa. Maswali matatu ya msingi kwa ajili ya kufanyia tathmini sehemu ya Kujenga Daraja ambayo umetengeneza: • Je ina ubunifu na inasisimua? • Je inalenga mahitaji na matarajio ya kundi husika? • Je inawaongoza watu kuelekea kwenye somo na inaibua shauku yao kuhusiana na somo hilo? Kwa mara nyingine, pitia Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na kukusanya mawazo kwa ajili ya shughuli za uhusianishaji zinazofaa kwa maudhui ya somo. Kisha, tengeneza sehemu ya uhusianishaji ambao unasaidia wanafunzi kuunda muunganiko mpya kati ya kweli za somo na maisha (maana halisi) na wajadili mabadiliko mahususi katika namna yao ya kuamini, mtazamo au matendo ambayo yanatakiwa yatokee kama matokeo (kufanyia kazi). Unapopanga, uwe na tahadhari kidogo usitengeneza sehemu ya muunganiko ambao ni mahususi sana. Kwa ujumla sehemu hii ya somo inatikiwa ije kwa wanafunzi kama mwaliko wa ugunduzi wa pamoja kuliko kama zao la matokeo fulani ambayo yalishatarajiwa kabla.

Kuandaa Sehemu ya Uhusianishaji

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online