Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 5 9
Kiini cha kila sehemu ya uhusianishaji ni swali (au mfululizo wa maswali) ambayo yanauliza wanafunzi ni kwa namna gani kuijua Kweli kutabadilisha kufikiri kwao, mitazamo, na tabia (tumejumuisha na baadhi ya maswali ya sehemu ya uhusianishaji ili “kuwapa hamasa” wanafunzi wako na kuchochea kufikiri kwao, na kuwasaidia kutenegeneza maswali yao wenyewe yanayotokana na hali halisi za maisha yao). Kwa sababu haya ni mafunzo ya kitheolojia na kihuduma, mabadiliko ambayo tunayohitaji zaidi ni yale ambayo yanahusiana na wanafunzi kuwafundisha na kuwaongoza wengine katika muktadha wao wa huduma. Jaribu na lenga katika kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu eneo hili la kutendea kazi katika swali ambalo unalitengeneza. Sehemu ya uhusianishaji inaweza ikatumia mifumo mbalimbli. Wanafunzi wanaweza kujadili maana yake na namna ya kutendea kazi kwa pamoja katika kundi linaloongozwa na mkufunzi au katika makundi madogo madogo wakiwa na wanafunzi wengine (inaweza kuwa mjadala wa wazi au ukifuata mfumo fulani wa maswali yaliyoandaliwa kabla). Kutumia uchunguzi kifani pia kwa kawaida ni namna nzuri ya kuanzisha mijadala. Bila kujali njia iliyotumika, katika kipengele hiki mkufunzi na kundi linalojifunza, wote lazima wafanyike chanzo cha hekima. Kwasabau wanafunzi wenyewe tayari ni Viongozi wa Kikristo, huwa kuna utajiri mkubwa wa maarifa na uzoefu ambao unaweza kupatika kutoka kwa wanafunzi wenyewe. Wanafunzi wanatakiwa kushauriwa kujifunza wao kwa wao lakini pia kutoka kwa Mkufunzi. Kanuni kadhaa zinatakiwa kuongoza mijadala ya sehemu ya uhusianishaji unayoiongoza: • Kwanza, lengo la msingi katika sehemu hii ni kuibua maswali ambayo wanafunzi wanayo. Kwa maneno mengine, maswali yanayojitokeza kwa wanafunzi wakati wa somo ndio yanapewa kipaumbele kuliko yale maswali ambayo mkufunzi ameyaandaa kabla – japokuwa maswali yalilotengenezwa na mkufunzi bado yatakuwa nyenzo muhimu sana za kujifunzia.
Sambamba na hili ni muhimu kufikiria kwamba swali linaloulizwa na mwanafunzi mmoja mara nyingi ni swali ambalo yumkini linaweza kuwepo kwa kundi zima.
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online