Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
6 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
• Pili, jaribu kuelekeza mjadala kwenye vitu halisi na mahususi kuliko vile vya kinadharia au kidhahania zaidi. Sehemu hii ya somo imekusudiwa kulenga kwenye hali halisi za maisha ambazo zinawakumba wanafunzi fulani katika darasa lako. • Tatu, usiwe na hofu kueleza hekima uliyoipata kupitia huduma yako mwenyewe. Wewe ndiwe nyenzo kuu kwa wanafunzi na hivyo wanategemea kwamba yale masomo ambayo umejifunza na wao watayapata pia. Hata hivyo,siku zote weka akilini kwamba tofauti ya tamaduni, muktadha, na haiba zinaweza kufanya kile ambacho kilifanya kazi kwako, kisifanye kazi marazote kwa kila mmoja. Tengeneza mapendekezo, lakini jadili na wanafunzi kama uzoefu wako unaweza kufanya kazi katika muktadha wao na kama hapana, ni nini kinaweza kurekebishwa ili ufanye kazi na kwao pia. Maswali matatu yenye manufaa kwa ajili ya kutathmini sehemu ya uhusianishaji uliyoutengeneza ni haya: • Nimepata picha mapema kuhusu maeneo ya jumla ya uhusianishaji na utendeaji kazi katika somo hili? • Nimetengeneza namna ya kuibua maswali ya wanafunzi yapewe uzito na kuyapa kipaumbele? • Je hii itasaidia mwanafunzi kutoka darasani akiwa anajua nini cha kufanya kutokana na ile kweli waliyojifunza? Mwisho, kwa sababu kazi ya huduma ni kazi ya utendaji katika mfumo maalum kwa kozi nzima, itasaidia sana kutenga pembeni sehemu ya uhusianishaji na kufanya wanafunzi wajadili nini wangeweza kuchagua kwa ajili ya kazi yao na kutathmini maendeleo na/au ripoti kwa darasa baada ya kumaliza kazi.
Shughuli za Ufunguzi
Hatua katika Kuongoza Kipindi
• Chukua mahudhurio • Ongoza ibada • Tamka au imba Kanuni ya Imani ya Nikea na kuomba
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online