Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 6 1

• Hakiki maagizo ya kukariri Maandiko • Kusanya kila kazi ambayo imeshafika muda wake.

Fundisha Kipengele cha Kujenga Daraja • Tumia mfano wa sehemu ya Kujenga Daraja uliyopo katika Mwongozo wa Mkufunzi au tengeneza wa kwako mwenyewe.

Simamia Kipengele cha Maudhui • Wasilisha Maudhui ya somo kwa kutumia mafundisho ya video.

Kutumia Video Kila somo lina vipengele viwili vya video, kila video moja ina urefu wa dakika kama 25. Baada ya kufundisha sehemu ya kujenga Daraja (ikijumuisha kauli ya mpito), onyesha kipengele cha kwanza cha video kwa ajili ya wanafunzi. Wanafunzi wanaweza kuendelea kujifunza na kuandika yale wanayojifunza kutumia Kitabu cha Mwanafunzi ambacho kina muhtasari wa kile kinacho onyeshwa katika marejeo ya Maandiko na nyenzo nyingine ambazo zinatumiwa na yule mzungumzaji kama marejeo. Baada ya kuwa sehemu ya kwanza imetazamwa, ongea na wanafunzi kuthibitisha kama kweli kile kilichoonyeshwa kimeeleweka. Kuhakikisha kuwa Maudhui Yanaeleweka Kwa kutumia Mwongozo wa Mkufunzi, chunguza ufahamu kwa kuuliza maswali yaliyo orodheshwa katika sehemu ya “Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu”. Fafanua kila eneo la uelewa ambalo wanafunzi wameonyesha kutolielewa vizuri kupitia majibu yao. Waulize wanafunzi kama kuna maswali yoyote ambayo wanayo kuhusiana na maudhui kisha myajadili pamoja kama darasa. Zingatia: maswali hapa yanatakiwa yahusu zaidi maudhui yaliyotazamwa na sio namna ya kutendea kazi kile

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online