Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

7 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

pamoja na wengine na kwa ajili ya wengine, wanaweza kujikuta wao wenyewe wamekauka na kuishiwa, endapo watakosa kulishwa vizuri na kuelimika kiroho. Ibada hii inalenga katika hazina ya ajabu ambayo ni Neno la Mungu, na inatupa changamoto ya kulizingatia kwanza kama chakula chetu na chanzo cha maisha yetu wenyewe, kisha kama silaha ya lazima katika huduma. Katika nyanja zote za maisha na huduma, hakuna kitu kinachotoa nguvu, kutia moyo, na kuleta burudiko kama Neno la Mungu. Sala hizi hazipaswi kuonekana kuwa sehemu tu ya somo bali kama kiashiria cha kihistoria na cha kiroho cha shauku tuliyo nayo ambayo Mungu hutuwezesha kulifahamu na kulitumia Neno Lake. Ni Mungu pekee, kupitia Roho wake, ndiye anayeweza kutuwezesha kuona na kuthamini Neno lake takatifu ipasavyo. Wahimize wanafunzi kumtegemea Bwana ili awasaidie kuelewa nguvu ya Neno liumbalo. Kipengele cha Kujenga Daraja hutafuta kuunda mazingira ambayo wanafunzi wanaweza kuanza kusikiliza uwasilishaji unaofuata. Kipengeke cha Kujenga Daraja kimekusudiwa kuwasaidia wanafunzi kutafakari juu ya kazi ya Neno la Mungu katika hali mbalimbali, umuhimu na kufaa kwake, na jukumu lake katika kushughulikia masuala na kutatua matatizo. Tumia kipengele hiki kuwasaidia wanafunzi kujadili kazi ya Maandiko katika mazingira mbalimbali muhimu katika jamii na maisha yao. Nguvu ya uumbaji ya Neno la Mungu inaonekana kwa hakika na kiroho katika somo hili, na mjadala wako unapaswa kuangazia kipengele hiki chenye nguvu cha Maandiko. Ukweli kwamba Neno la Mungu lina nguvu maalum katika uumbaji wa Mungu labda ni muhtasari bora zaidi katika Zaburi 147:15-20: Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana. 16 Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu, 17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama? 18 Hulituma neno lake

1

M A F U N Z O Y A B I B L I A

 4 Ukurasa wa 84 Kanuni ya Imani ya Nikea

 5 Ukurasa wa 85 Kujenga Daraja

 6 Ukurasa wa 93 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online