Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 7 1
na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka. 19 Humhubiri Yakobo neno lake, Na Israeli amri zake na hukumu zake. 20 Hakulitendea taifa lo lote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya! Andiko hili linaangazia kanuni ambayo inafaa kujadiliwa kwa kina na kueleweka katika wakati wako wa maswali na majibu. Zilizo orodheshwa katika sehemu hii ni kweli za msingi zilizoandikwa kwa namna ya sentensi ambazo wanafunzi walipaswa kuwa wamepokea kutokana na somo hili, yaani, kutoka kwenye video na mjadala wako wenye mwongozo pamoja nao. Usisite kurudia dhana au kweli kwa msisitizo. Hakikisha kuwa dhana hizi zimefafanuliwa wazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwa sababu kazi yao ya jaribio na mitihani itachukuliwa kutoka kwenye vitu hivi moja kwa moja. Muhimu zaidi, tafuta kutumia muda vizuri ili ujue kwamba wanafunzi wanaelewa mawazo haya ya msingi ambayo yanafafanua somo hili. Katika kuwasaidia wanafunzi wako kufikiria kupitia hali zao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali au kutumia yale yaliyotolewa hapa chini ili kuchochea shauku zao. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, lakini kwako, katika mazungumzo na wanafunzi wako, kutatua kada ya masuala, wasiwasi, maswali, na mawazo ambayo hutiririka moja kwa moja kutoka kwenye uzoefu wao, na kuhusiana na maisha na huduma zao. Tunachotafuta hapa ni kushughulikia maswala muhimu ambayo wanafunzi huibua kutokana na maswali na wasiwasi walizo nazo, hasa yale wanayoona yanaendana zaidi katika muktadha wa huduma yao hivi sasa. Lengo la sehemu hii ni wewe kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na mazingira ya huduma. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama mahitaji kamili. Chukua na uchague kati yake, au uje na yako mwenyewe. Jambo kuu sasa ni kule kuendana, kwa hivyo uwe wazi sana kwao ukifafanua masuala na kubainisha maswali unayojibu sasa hivi.
1
7 Ukurasa wa 93 Muhtasari wa Dhana Muhimu
M A F U N Z O Y A B I B L I A
8 Ukurasa wa 94
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online