Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

7 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Asili ya mifano halisi ni kuwawezesha wanafunzi kutumia kwa ubunifu ukweli ambao wamekuwa wakijadili kwa hali halisi au hali za kufikirika. Hakuna majibu sahihi kwa maana ya kwamba njia moja tu inaweza kuamua namna ya kuyashughulikia au kuyaelewa. Unachotafuta kupitia uzingatiaji wako wa haya ni uwezo wa wanafunzi kuunganisha masomo yao na hali halisi za huduma ambazo zitadai utambuzi wao, tiba, na ubashiri wa masuala na changamoto za kiroho. Katika uhalisia, mifano halisi inahusu utatuzi wa matatizo, kwa hivyo wasaidie wanafunzi kutafuta kuunganisha mafunzo yao na masuala makuu yanayoendelea kwenye hali hiyo. Acha wanafunzi watenge masuala yanayohitaji kutatuliwa, na waeleze kanuni za kibiblia zinazohusiana na maoni yao. Wasaidie kueleza misimamo yao kwa uwazi, na kuhimiza mwingiliano na wanafunzi na kweli za masomo. Kila somo humruhusu kila mwanafunzi kuona namna kweli za somo husika zinavyohusiana na kutumika kimaalum katika maisha na huduma yake. Bila shaka, kanuni unazoshughulikia zinahusiana na maisha ya wanafunzi, na ikiwa unajua ni kwa jinsi gani, unaweza kuzisisitiza, au kuwasaidia wanafunzi kuona uwiano huo, na kujibu ipasavyo kama wanaweza. Matumizi ya Neno la Mungu kwa maisha yao binafsi ndilo lengo la sehemu hii. Wahimize wanafunzi kutafakari juu ya maisha yao ya binafsi ili kuona jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kuwataka kutumia kweli hizi katika maisha yao wiki hii. Patikana, ikiwa muda unaruhusu, kwa ajili ya ushauri na maombi maalum ambayo wanafunzi wako wanaweza kuwa nayo katika maisha na huduma zao. Lengo la elimu yote ya kitheolojia na misiolojia ni kuwawezesha wanafunzi kibinafsi kufanya Neno la Mungu kuwa hai katika maisha yao binafsi na kupitia wao katika makusanyiko yao na huduma zinazobubujika kutoka kwao. Namna unavyowafahamu kibinafsi wanafunzi, na uwazi wao kwako unapaswa kukupa nafasi ya kuwashauri kwa kiwango fulani. Usilazimishe, lakini uwe tayari kwa hilo, na ulitarajie. Maandiko yatawafanya wanafunzi wako wawe wazi kwa Mungu na mpango wake, kwa hivyo utayari wako wa kusaidia kimaalum na kwa uthabiti ni sehemu muhimu ya jukumu lako la ushauri. Wakumbushe

 9 Ukurasa wa 95 Mifano Halisi

1

M A F U N Z O Y A B I B L I A

 10 Ukurasa wa 97 Kuhusianisha Somo na Huduma

 11 Ukurasa wa 97 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online