Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 7 3
wanafunzi kwamba Neno la Mungu ni kwa ajili ya matumizi, na sio tu kutafakari na majadiliano (Yak. 1:22-25). Roho Mtakatifu na akuongoze unapowasikiliza na kuwajibu wanafunzi wako.
Usimamizi wa maelezo ya kozi, pamoja na kuhifadhi kumbukumbu na mawasiliano mazuri, ni sehemu kuu ya jukumu lako kama mshauri. Pamoja na mistari hii, ni muhimu uhakikishe kwamba wanafunzi wanaelewa zoezi la wiki inayofuata, hasa yale yaliyoandikwa. Hii sio ngumu; lengo ni kwamba wasome nyenzo kwa kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile wanachodhani kimemaanishwa. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao ujuzi wao hufanya hili kuwa mzigo na /au vigumu, wahakikishie kwamba dhamira ya kazi hii ni kuwahimiza kuelewa nyenzo, na si kuonyesha ujuzi wao wa kuandika. Ingawa uboreshaji wa ujuzi wa kuandika ni lengo linalofaa, hatutaki kusisitiza ujuzi kama huo kama mbadala wa kuwatia moyo na kuwajenga. Wala, hata hivyo, hatutaki kuwapuuza. Pambana ili kupata mpenyo kati ya changamoto na kutia moyo.
12 Ukurasa wa 98 Kazi
1
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online