Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 7 5

Ufasiri wa Biblia Mbinu ya Hatua Tatu

SOMO LA 2

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 2, Ufasiri wa Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu . Lengo la jumla la somo hili ni kuwapa wanafunzi mbinu bora, inayotenda kazi na inayozingatia wakati na muktadha katika ufasiri wa Biblia ambayo itawaruhusu wao kukua katika ujuzi wao wa kutafsiri Maandiko kwa usahihi ( exegesis ). Utawaongoza wanafunzi katika kanuni za msingi zinazolenga katika umuhimu wa Biblia, lakini sio mbinu ambayo inahimiza ama mashaka au kutegemea sana njia na mbinu za kisayansi na mbinu nyingine za aina hiyo. Kama ilivyotajwa katika somo lililopita, mbali na kazi ya Roho Mtakatifu ya kutia nuru, hakuna mtafsiri yeyote wa Biblia anaweza kuelewa ufahamu na mawazo ya Mungu kuhusiana na jambo lolote, achilia mbali kusudi la kimungu la wokovu katika Kristo Yesu (1 Kor. 2.9-16). Hata hivyo, tunahitaji kutumia mbinu, katika kufasiri Maandiko, ambazo si za kubahatisha au za kiholela. Mbinu ya Hatua Tatu imetengenezwa ili kuwasaidia wanafunzi wako kwanza waone uhitaji wa mbinu hiyo na kisha kuwa mahiri katika kuitumia. Kwa njia fulani, mbinu hii sio mpya, bali ni mwendelezo na upanuzi zaidi wa kanuni za msingi katika utafsiri wa Maandiko unaofahamika na wanazuoni kwa miaka mingi. Kanuni ya kwanza ni umuhimu wa kuitafsiri fasihi , ambayo kimsingi ina maanisha kwamba maneno na sentensi zilizopo kwenye Biblia zinatakiwa kueleweka, kwanza kabisa, kwa maana za kawaida , isipokuwa tu kama maana hiyo haileti maana kwa sasa! Pamoja na msaada wa kitheolojia na matumizi ya lugha, lengo letu ni kuisoma Biblia kama kitabu kingine chochote cha kifasihi, ndiyo maana, tunataka kuelewa maneno kama yanavyoeleweka katika mawasiliano ya kawaida. Mbinu ya Hatua Tatu inazingatia sana nguvu ya lugha kama chombo cha Mungu katika kuwasiliana nasi kupitia Mwana wake na Roho Mtakatifu, na inathibitisha ushahidi katika Maandiko yenyewe kwamba unabii wa Agano la Kale ulitafsiriwa kwamba ni wa kweli katika vifungu vya Maandiko kama Zaburi 22, Isaya 7.14 na Mika 5.2. Utagundua pia, kwamba muundo na asili ya lugha umezingatiwa sana na Mbinu ya Hatua Tatu, kwa maneno mengine, inaweka umakini wa karibu sana kwenye uhusiano wa kisarufi kati ya maneno yaliyopo kwenye andiko na namna ambavyo neno halisi linafanya kazi kisintaksia katika uhusiano wa moja na jingine. Mbinu hii inathibitisha dhana ya “Uvuvio wa Jumla” wa Maandiko, ambao

 1 Ukurasa wa 101 Utangulizi wa Somo

2

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online