Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
7 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
unasisitiza kuwa maneno (yenye kuzungumzwa) na Maandiko kwa ujumla wake (kila neno) yamevuviwa kikamilifu na Roho Mtakatifu, na kwa sababu hiyo lazima tu tutazame usahihi wa namna maneno yalivyopangiliwa katika sehemu ya andiko na Maandiko yote kwa ujumla. Sheria za msingi za lugha na fasihi zote zinatumika katika uhusiano wa kisarufi wa Maandiko, na hivyo inakuwa ni muhimu kuweka umakini wa karibu katika maneno na sheria ambazo zinaviunganisha pamoja. Kutokana na kwamba Mbinu ya Hatua Tatu inalenga sana katika umuhimu wa kuziba mwanya uliopo kati ya ulimwengu ule wa kipindi Maandiko yanaandikwa na huu wa sasa, mbinu hii imeundwa katika hali ya kuhitaji kuelewa andiko katika hali yake ya asili, yaani muktadha wake wa kihistoria wa mwanzo kabisa. Mungu aliongea na watu wake kupitia matukio, maneno, kujidhihirisha kwao na namna nyingine mbalimbali kama zinavyoelezewa kwenye Neno la Mungu. Kama waamini katika nguvu za Roho Mtakatifu, kuendelea kutumia Neno katika maisha yetu, kunatufanya tuzidi kugundua kile ambacho andiko lilimaanisha katika muktadha wake wa kihistoria ili kupata ufahamu wa nini andiko linamaanisha kwetu leo. Kusudi letu katika Mbinu ya Hatua Tatu , ni kutokufanya makosa ya kihistoria au ya kisarufi ambayo yanaweza kutufanya kutafsiri tofauti maana ya andiko katika muktadha wake wa awali, na ili tusiitumie vibaya maana yake katika muktadha wetu leo. Hatimaye, tunathibitisha Biblia kama kitabu cha kifasihi, na kwasababu hiyo, kinatakiwa kisomwe katika muktadha wa mgawanyiko wake katika muktadha wake wa kifasihi. Kwasababu Biblia kiuhalisia ni maktaba ya maandishi ya kazi mbalimbali za kifasihi, baadhi ya maarifa ya namna aina fulani za fasihi zinafanya kazi zinamsaada sana katika kutambua maana ya ujumbe kupitia tanzu za kifasihi na katika muktadha wa fasihi. Mbinu ya Hatua Tatu, inatazama muktadha wa kifungu cha Maandiko kuhusiana na aya zinazotangulia na aya zinazofuata kifungu husika. Vilevile tutaangalia kifungu cha Maandiko kulingana na muktadha wake chenyewe, nafasi yake katika sehemu ya sura au kitabu na tutajitahidi kupata maana ya andiko kulingana na nafasi yake katika kazi nzima. Hata baada ya masuala haya muhimu ya kimuktadha kuwa yameshugulikiwa, bado tutawahimiza wanafunzi kuwa bora katika
2
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online