Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 8 1
Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake Kutolewa kwa Ahadi Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 3, Ushahidi wa Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme Wake: Kutolewa kwa Ahadi . Lengo la jumla la somo hili ni kuwasaidia wanafunzi wako kuona jinsi ambavyo Agano la Kale, kwa ukamilifu na ushawishi, linazungumza kuhusu Masihi kama alivyofunuliwa katika nafsi ya Yesu Kristo. Tasnifu ya somo hili itakuwa kuonyesha kwamba mada ya Agano la Kale ni utambulisho wa Kristo, na kutoa mwangaza wa tabia, kazi, na utukufu wa Masihi ajaye, na linafanya hivi kwa njia na namna mbalimbali. Katika uhalisia, Agano la Kale ni kivuli na utabiri wa yule ajaye, likimfunua katika historia ya Israeli, katika mifano ya kimahusiano na wahusika mbalimbali wa Agano la Kale katika taasisi na matukio yake, na katika haki na unabii wa Kimasihi kuhusu Mkombozi na mpakwa mafuta ajaye. Kimsingi, somo hili linahusu hemenetiki , yaani, jinsi tunavyopaswa kusoma na kufasiri Agano la Kale kwa njia inayolingana na mshikamano na muundo wake wa ndani. Kwa wanafunzi wengi wa Biblia, wa mijini na kwenye vitongoji, tunaona leo hii kupuuzwa kwa jumla kwa maandiko ya Agano la Kale na kutokuwa na ufahamu wa sehemu hiyo muhimu ya Maandiko Matakatifu. Na haishangazi: Agano la Kale ni mkusanyiko wa fasihi tofauti tofauti, zinazohusiana na watu na tamaduni fulani za kale, na mara nyingi linawasilisha ujumbe wake kwa lugha ya kitamathali na ya ishara. Limejikita zaidi katika historia endelevu ya watu wa Israeli, na uhusiano kati ya Mungu na watu hawa kama taifa ambalo Masihi wake mwenyewe angetokea kama Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu. Hoja itakayo simamiwa katika somo hili ni kwamba somo muhimu la Agano la Kale ni uhusiano wake na Masihi aliyefunuliwa katika Yesu Kristo katika Agano Jipya. Msukumo huu uletao hisia ya kumtarajia Masihi katika Agano la Kale unatengeneza muunganiko wa karibu na msukumo unaolingana nao katika Agano Jipya, ambao ni ufunuo wa Masihi kama Yesu wa Nazareti. Uhusiano wa Agano la Kale na Agano Jipya ni uhusiano wenye msingi kimahususi katika Kristo: Agano la Kale linatoa msingi wa tumaini na ahadi ya Masihi ambayo imefunuliwa na kufafanuliwa katika Agano Jipya. Kwa maana hii, hatuwezi kulielewa Agano la Kale peke yake ; bila kulitafsiri kwa msingi wa namna linavyonukuliwa na kutumiwa katika Agano Jipya . Kwa upande wa historia ya Israeli, ule mkazo juu ya sherehe na ibada za kidini, mafundisho yake
SOMO LA 3
1 Ukurasa wa 133 Utangulizi wa Somo
3
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online