Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

8 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

ya kiwacho cha juu kuhusu maadili, na utabiri wake kwa habari ya Masihi ajaye, Agano la Kale linatoa msingi wa kuielewa na kuithamini huduma ya Yesu. Umoja huu muhimu na mwendelezo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya ndio kanuni inayoendekesha na kuongoza kozi hii. Tutatumia Agano Jipya kuleta maana ya Agano la Kale, na Agano la Kale kufafanua na kuangazia ujumbe wa Agano Jipya. Mwendelezo na umoja huu ndio msingi wa uhusiano kati ya maagano haya. Norman Geisler, ambaye bila shaka ameandika baadhi ya hoja zenye nguvu na ushawishi zaidi kuliko msomi yeyote wa Biblia juu ya umoja na mwendelezo kati ya maagano haya, anaweka wazi uhusiano huu kati ya Agano la Kale na Jipya. Anajibu vizuri swali, “Ni ipi njia sahihi ya kufasiri Biblia?”: Ni ipi njia sahihi ya kufasiri Biblia? Wakati fulani inafikiriwa kwamba kuna tafsiri nyingi tofauti za Biblia kama vile wasomaji wake walivyo wengi. Biblia inapaswa kuelewekaje? Kama vile towashi Mwethiopia alivyouliza, akiwa na Biblia mkononi, “Ninawezaje [kuelewa] mtu asiponiongoza?” Jibu la tatizo hili kwa Mkristo liko wazi. Kristo ndiye kiongozi wetu; yeye ndiye ufunguo wa tafsiri ya Biblia. Yesu alitamka mara tano kwamba yeye ndiye ujumbe mzima wa Maandiko ya Agano la Kale. Akizungumzia Sheria na Manabii alisema, “Sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Mt. 5:17). Yesu alitembea na wanafunzi wawili katika njia ya kwenda Emau, na “akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” (Lk 24:27). Baadaye, kwa wanafunzi kumi katika chumba cha juu Yesu alisema, “Yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimizwe” (Lk 24:44). Katika mazungumzo na Wayahudi Yesu aliwaambia hivi: “Mnachunguza Maandiko . . . na hayo ndiyo yanayonishuhudia” (Yn. 5:39). Mwandishi wa Waebrania anathibitisha maneno haya ya Zaburi 40 kwamba yanamhusu Kristo: “Katika gombo la chuo nimeandikiwa” (Ebr. 10:7). Mara hizi tano Bwana wetu alithibitisha kwamba yeye ndiye ujumbe wa Agano la Kale lote. Tunaweza kuhitimisha basi, kwa mamlaka ya Kristo, kwamba yeye ndiye ujumbe mkuu wa Biblia nzima. Biblia lazima itafsiriwe katika msingi wa Kristo (yaani, Kristo akiwa ndiye msingi mkuu). Hakuna namna nyingine kwa Mkristo kuielewa. Kuna angalau namna tatu za msingi ambazo kwazo tunaweza kumwona Kristo katika Biblia tunapochunguza yaliyomo: (1) Kristo

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online