Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 8 3
ndiye ujumbe wa maagano yote mawili ya Biblia, (2) Kristo ndiye ujumbe wa kila sehemu moja katika sehemu nane za Maandiko, na (3) Jumbe na kweli zinazomhusu Kristo zinaweza kupatikana katika kila moja ya vitabu sitini na sita vya Biblia. Kama mchezo wa fumbo, mara picha ya jumla (ujumbe) inapoeleweka, ni rahisi zaidi kuweka vipande vyote pamoja.
~ Norman L. Geisler. A Popular Survey of the Old Testament . Grand Rapids: Baker Book House, 2003. uk. 19-20.
Geisler anatoa muhtasari wa kile kitakachokuwa mada ya msingi ya somo hili. Tunatumai kwamba wanafunzi wako hawatatishwa na Agano la Kale, badala yake wataona kwamba kwa kule kuwa na mkazo juu ya Kristo, wanaweza kuelewa ujumbe wa Agano la Kale. Kwa kuuelewa muundo wake katika namna inayomlenga Kristo, wanaweza kuanza kuelewa ujumbe wake wa msingi na hatimaye kufahamu muundo wake wa ndani kwa njia ambayo mbinu za kawaida za kujifunza Agano la Kale haziwezi. Kupitia somo hili lote, utatakiwa basi kuwatia moyo wanafunzi wako katika uwezo wao wa kuuelewa muundo muhimu na data zinazounda toleo kubwa lenye fasihi tofauti tofauti tunaloliita Agano la Kale. Mkazo huu juu ya hemenetiki yenye msingi wa Kristo ndiyo namna ambayo watu wasio wataalam katika lugha na utamaduni wa Agano la Kale wanavyoweza kupata ujuzi halisi wa kina wa mantiki na kanuni zilizomo ndani ya kitabu chochote cha AK. Hata hivyo, kusema tu hili, hakutakuwa na ushawishi hadi pale wanafunzi wako watakapopata fursa ya kuona jinsi kanuni hii inavyofanya kazi katika fasihi husika. Somo hili limeundwa ili kuonyesha ni kwa jinsi gani ulivyo wa kina uhusiano kati ya mafundisho ya Agano la Kale na nafsi na kazi ya Yesu Kristo. Mkazo huu juu ya umoja wa Maandiko, ambao unatupatia uwezo wa kuelewa maana ya jumla na matumizi yake, ndiyo mada muhimu ya somo. Yasisitize mara nyingi uwezavyo, na utumie mifano ya hemenetiki yenye msingi wa Kristo ambayo imetolewa hapa kama ushahidi wa yote mawili. Mwanzoni mwa kila somo utagundua kwamba madhumuni na malengo ya somo yameonyeshwa kwa uwazi. Malengo haya yanawakilisha kiini cha maarifa na msukumo ulio nyuma ya uwasilishaji na majadiliano ya somo. Tumejaribu kuyaweka kwa namna iliyo wazi na ya moja kwa moja. Unapaswa kuyasisitiza
3
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online