Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

8 4 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

katika somo lote, wakati wa majadiliano na muda wa uwepo wako na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo haya katika kipindi chote cha darasa, ndivyo utakavyoongeza uwezekano wa wanafunzi wako kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo husika. Kwa mara nyingine tena, malengo yanawakilisha “ujumbe wa ziada” wa somo (yaani, mawazo yale ambayo, baada ya yote kusemwa na kufanyika, tunataka wanafunzi wabaki nayo). Unapaswa kutumia muda wa kutosha kuyapitia kabla ya kipindi cha darasa, na uongoze tukio zima la kujifunza kwa kujadili malengo ya somo na umuhimu wake. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi. Vuta umakini wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, katika maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyaangazia haya kila mara, ili kuyasisitiza na kuyakazia tena na tena kadri unavyoendelea. Ibada hii inasisitiza ahadi ya Mungu kama msingi na kiini cha muundo na maisha ya Agano la Kale, na utimilifu wake katika Agano Jipya. Njia inayoaminika, rahisi na ya kuvutia zaidi ya kuunda mfumo wa uelewa wetu wa mafundisho ya Biblia ni kupitia dhana ya ahadi na utimilifu . Tangu mwanzo, Mungu alitangaza kwamba angemtuma Mwokozi ambaye mara moja na kwa wakati wote angerekebisha hali iliyotokea kwa sababu ya uasi wa hiari na usio na maana wa wazazi wetu, Adamu na Hawa, na mapinduzi yasiyo na maana ya Shetani dhidi ya mamlaka na utawala wa Mungu. Ahadi hii na utimilifu wake vinawakilisha muundo wenyewe hasa wa ufunuo wa Biblia, na kuweka wazi uhusiano kati ya Agano la Kale (kama kielelezo cha ahadi), na Agano Jipya (kama ufafanuzi na utimilifu wake). Neno la Kiingereza “ promise ” yaani, ahadi, linahusiana na neno la Kilatini promissa , linalofafanuliwa katika Kamusi ya Oxford kama “tangazo au uhakikisho unaotolewa kwa mtu mwingine kuhusiana na wakati ujao kwa kueleza kwamba mtu atafanya au kujiepusha na jambo fulani lililotajwa, kwa kawaida katika maana njema kwa ajili ya manufaa au furaha ya mhusika.” Ingawa lugha ya Kiebrania haionekani kuwa na neno linalowasilisha maana hii hasa, wazo

 2 Ukurasa wa 133 Malengo ya Somo

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

 3 Ukurasa wa 134 Ibada

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online