Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 8 5

la ahadi liko wazi katika matumizi ya neno dabar , linalotafsiriwa katika mamia ya maeneo tofauti tofatui katika maana ile ile kama tunavyolitumia leo, yaani, ahadi zilizotolewa baina ya watu, au zile zilizofanywa na Yehova kwa watu wake (Kum. 1:11; 6:3; 9:28; 15:6; 19:8, 1 Fal. 5:12, nk). Kuelewa vyema asili ya ahadi katika rekodi ya Biblia kunaweza kukusaidia katika mazungumzo yako na wanafunzi. Kwa mfano, neno angelia ni neno linalotumika kama tafsiri ya neno “promise” (ahadi) katika Agano Jipya. Katika maeneno mengi sana hutafsiriwa tu kama “ahadi,” kama nomino na inapotumiwa katika hali yake kitenzi. Katika namna ya kufurahisha, neno angelia linamaanisha “jambo linalotangazwa.” Moja ya maneno yanayofanana nalo ni angelos (ambalo kwalo tunapata neno “angel,” yaani “malaika”, yule anayetangaza au kuleta ujumbe). Neno la Agano Jipya la Injili euangelia linamaanisha ujumbe au tangazo la habari njema. Katika matukio machache linatumika kuhusiana na ahadi zilizofanywa baina ya watu (rej. Mdo. 23:21). Hata uchunguzi wa hatikunjo za Agano la Kale, maandishi ya kale zaidi yanaonyesha umuhimu wa ahadi uliopo ndani yake, hasa kuhusu ahadi ya Mungu ya kumpa Ibrahimu mrithi (taz. Rum. 4:13-16, 20; 9:8-9; 15:8; Gal. 3:16-22; 4:23; Ebr. 6:13-17; 7:6; 11:9, 11, 17). Ahadi hizi hutoa muundo na sura ya historia nzima na maisha ya Ibrahimu, warithi wake (yaani, wazao wake Isaka na Yakobo), na watu ambao wangetokana nao kubeba tumaini la uzao wa Ibrahimu ambao ulikusudiwa kuleta ukombozi na urejesho kwa watu na nchi ile. W. M. Smith anaangazia umuhimu wa dhana ya ahadi katika mjadala wa utabiri wa Mungu wa kinabii kwamba atamtuma mrithi kama ahadi yake kwa Ibrahimu na mzao atakayeketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi, «Mwokozi kulingana na ahadi» (Mdo 13:23): Stefano anazungumza juu ya wakati wa kujiliwa kama “wakati wa ahadi kukaribia” (Mdo 7:17). Ahadi hii ya Mwokozi kwa Daudi imethibitishwa katika Kristo (Mdo 13:32). Ni katika kundi hili la ahadi tunapswa kuweka dokezo la Paulo la “ahadi kwa imani katika Yesu Kristo” (Gal. 3:22). Inawezekana kwamba mgawanyiko huu wa ahadi katika makundi mawili, zile zilizotolewa kwa Ibrahimu kuhusu uzao na zile alizopewa Daudi kwa habari ya mfalme

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online