Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
8 6 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
atakayetawala, zimeunganishwa katika marejeo ya Paulo kuhusu mada hii kama “ahadi walizoahidiwa mababa” (Rum. 15:8); katika mjadala uliozoeleka wa wakati ujao wa Israeli, anawataja Waisraeli kama “watoto wa ahadi” (Rum. 9:8-9) na kuwakumbusha kwamba wao ndio walio na ahadi za Mungu (Rum. 9:4). Inayohusiana kwa ukaribu na hii ni zawadi ya Mungu aliyotuahidia katika Kristo, yaani, ahadi ya uzima katika Kristo (2 Tim. 1:1), au, kama inavyoonyeshwa mahali pengine, “ahadi ya urithi wa milele” (Ebr. 9:15) au kama Yohana alivyoandika, “ahadi ile aliyotuahidi, ndiyo uzima wa milele” (1 Yoh. 2:29). ~ W. M. Smith. “Promise.” The Evangelical Dictionary of Theology . Walter A. Elwell, mh. (toleo tepe). Ellis Enterprises, Inc. Grand Rapids: Baker Book House, 1984. Kiini cha wokovu wetu kimejikita katika uaminifu wa Mungu wa kutunza ahadi zake kwa ulimwengu wake, kwa wanadamu, kwa rafiki yake Ibrahimu, na kupitia yeye, kwa wale wote wanaomwamini Yesu wa Nazareti kama Masihi na Bwana, utimilifu wa ahadi ya kiungu. Katika uhalisia, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ndiye Mtimiza-Ahadi wa kwanza, yule aliyeapa kwa nafsi yake mwenyewe kujipatia watu kutoka duniani ili wawe milki yake mwenyewe. Mwandishi wa Waebrania anasema kwamba ujuzi huu wa uaminifu wa Mungu kwa ahadi yake ni nanga ya nafsi zetu, msingi wa uhai wetu: Ebr. 6:17-19 - Kwa hiyo Mungu alipotaka kuwahakikishia warithi wa ahadi yake kuhusu makusudi yake yasiyobadilika, aliwathibitishia kwa kiapo. 18 Mungu alifanya hivyo ili, kwa kutumia mambo haya mawili yasiyobadilika, na ambayo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tuliokimbilia usalama kwake tutiwe moyo, tushikilie kwa uthabiti tumaini lililowekwa mbele yetu. 19 Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho zetu yenye nguvu na imara. Tumaini hili linaingia hadi ndani ya pazia. Wakumbushe wanafunzi wako kwamba muundo wa agano unalingana kikamilifu na tabia ya Mungu aliye hai ambaye ahadi yake na utimilifu wake ni msingi na tegemeo la tumaini letu la uzima wa milele, na uhakika wa huduma zetu katika jina la Yesu.
3
M A F U N Z O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online