Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 8 7
Sehemu ya Kujenga Daraja katika masomo haya imeundwa ili kukusaidia “kuwachochea” wanafunzi wako kabla ya kuwashirikisha maarifa kupitia uwasilishaji wa somo na mijadala hapo baadaye. Sehemu hizi zimeundwa ili kukupa fursa ya kuitambulisha mada husika kwa wanafunzi wako, na kwa namna hii inakuwa njia ya vitendo, ya kuvutia, na/au yenye kuleta changamoto au chemsha bongo. Mifano ya kujenga daraja yenyewe ni vianzilishi vya majadiliano, vinavyokusudiwa kuelekeza umakini wa wanafunzi kwenye taarifa ambazo mnakaribia kujifunza. Kwa hivyo, ni daraja la kuingia kwenye maarifa yaliyomo katika somo, na si kiini cha somo lenyewe. Kwa maneno mengine, zitumie ili kuvutia umakini wa wanafunzi na kuwafanya wazingatie somo la siku hiyo. Hata hivyo, kuwa mwangalifu, ili usichukue muda mwingi wa somo lako katika kipengele hicho. Kimsingi kimekusudiwa kutambulisha somo, sio kuchukua nafasi ya somo. Kujadili maarifa ya somo pamoja na wanafunzi ni kipengele muhimu katika mchakato wa kujifunza ya kila somo. Maswali yafuatayo yameundwa ili kukusaidia kukagua dhana na mawazo makuu yaliyotolewa katika video. Unachopaswa kulenga kufanya ni kuwahusisha wanafunzi kikamilifu katika mawazo yanayoshughulikiwa, huku ukihakikisha kwamba wameelewa mawazo muhimu na uhusiano baina ya mawazo hayo. Unapozungumza na wanafunzi wako, usisite kuzifafanua dhana hizo kadiri unavyoendelea. Bila shaka mara kwa mara, watakutana na wazo au mada ambayo inawachochea na/au kuwatatiza. Zaidi ya haya, pamoja na wakati wako wote wa mazungumzo, itabidi upime muda wako vizuri, hasa ikiwa wanafunzi wako wanavutiwa na maarifa ya somo, na wanataka kujadili matumizi ya maarifa hayo kwa urefu. Zilizoorodheshwa hapa chini ni kweli za msingi zilizoandikwa kwa namna ya sentensi ambazo wanafunzi walipaswa kuwa wamepokea kutoka kwenye somo hili, yaani, kutoka kwenye video na mjadala ambao umeuongoza pamoja nao. Hakikisha kuwa dhana hizi zimefafanuliwa wazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwani majaribio na mitihani itachukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye maarifa haya.
4 Ukurasa wa 138 Kujenga Daraja
3
5 Ukurasa wa 147 Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu
M A F U N Z O Y A B I B L I A
6 Ukurasa wa 148 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online