Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
8 8 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Kusudi la sehemu hii ni kuwasaidia wanafunzi wako kutumia jumbe na kweli za Biblia katika maisha yao binafsi. Ni rahisi sana kwetu kujadili maarifa ambayo tumegundua katika uchunguzi wetu wa andiko na kisha kukosa kugundua maana yake kwa ajili ya maisha yetu wenyewe. Sehemu hii katika kila somo ni fursa kwetu kuhusianisha kweli hizi na maisha yetu wenyewe na namna tunavyotembea na Bwana . Katika kuwasaidia wanafunzi wako kutafakari mazingira yao wenyewe, unaweza kubuni baadhi ya maswali ili kuwasaidia kutumia kweli za somo hili katika maisha yao. Jisikie huru kutumia maswali yote au baadhi ya maswali yaliyotolewa hapa chini kama njia ya kuendeleza mazungumzo ili kufungua njia ya tafakuri ya pamoja kuhusu njia ambazo maarifa ya somo yanaweza kuwekwa katika vitendo. Kilicho muhimu hapa sio maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali ni wewe na wanafunzi wako, kupitia mijadala, kutatua kada ya masuala, hofu, maswali, na mawazo ambayo yanatokana moja kwa moja na uzoefu wa maisha yao, na kuhusiana na maisha na huduma zao. Usisite kutumia muda mwingi kwenye swali fulani linaloweza kuibuka kutokana na mafundisho au mambo fulani maalum ambayo yanaendana hasa na muktadha wa huduma yao wakati huu. Lengo la sehemu hii ni wewe kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao wenyewe na mazingira ya huduma zao. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyopo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama ya lazima. Chukua baadhi kati ya haya, au uje na yako mwenyewe. Jambo muhimu ni kwamba yaendane na muktadha wao wa sasa na maswali waliyo nayo. Mifano Halisi imeundwa ili kuwalazimisha wanafunzi kujihusisha katika matumizi ya kweli katika hali halisi au za kufikirika, ambazo zinawahitaji kuchukua kwa uzito uhusiano wa kweli hizo na matukio au masuala halisi. Jambo la msingi si kwamba wagundue “jibu sahihi” au “suluhisho sahihi” kwa hali hiyo, bali wajifunze jinsi ya kukusanya taarifa zote kwa umakini, kuzifikiria kwa umakini, na kuzitendea kazi kulingana na yale waliyojifunza. Mifano hii halisi, hata ile iliyobuniwa kutokana na hali za kufikirika, inaendana kwa karibu na aina ya masuala na hali ambazo viongozi wa mijini wanaweza kukutana nazo, hivyo wahimize kufikiri kama viongozi
7 Ukurasa wa 150
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
3
M A F U N Z O Y A B I B L I A
8 Ukurasa wa 152 Mifano Halisi
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online