Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 8 9

wanaposhiriki katika majadiliano. Huu sio uigizaji , bali ni mazoezi , na, kwa mujibu wa ule msemo, si sahihi kwamba mazoezi huleta ukamilifu; badala yake, mazoezi sahihi huleta ukamilifu zaidi.

Sehemu ya Kuhusianisha Somo na Huduma inaenda sambamba na sehemu ya Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi katika namna inayolenga matumizi ya moja kwa moja na mahususi ya somo katika mazingira na hali ya mwanafunzi. Hata hivyo, tofauti kuu ni kwamba sehemu ya Kuhusianisha Somo na Huduma inasisitiza kuhusu uwezo wao wa kufikiria ni jinsi gani kweli hizi zinavyohusiana na utendaji wao na utekelezaji wa huduma . Kwa maneno mengine, kusudi ni kuwasaidia wanafunzi kushughulika na matokeo ya kweli zinazofundishwa katika somo kwa kuzingatia namna ambazo kwa sasa wanatunza nafsi, kufundisha na kuhubiri, au kwa namna yoyote ya utumishi wao kwa Bwana. Tabia hii ya kutafuta kila mara namna za kutumia Neno la kweli maishani mwao ni msingi katika matumizi yao thabiti ya Biblia. Kumbuka kanuni hii kama ilivyoelezwa katika Agano Jipya: Ebr. 5:11-14 – Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya. Yak. 1:22-25 – Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

 9 Ukurasa wa 155 Kuhusianisha Somo na Huduma

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online