Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi
9 0 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I
Mt. 7:24-25 – Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Mt. 12:50 – Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu. Mt. 28:20 – . . . na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Lk 6:46-48 – Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? 47 Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. 48 Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lk 11:28 – Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika! Wakumbushe wanafunzi wako mara kwa mara kwamba kujifunza Neno la Mungu kunapaswa kupelekea katika badiliko la maisha yao na kufanywa upya nia zao (Rum. 12:2), si tu kujaza madaftari yao, na kukamilisha kazi zao! Wasaidie kuchunguza maeneo nyeti maishani mwao ili waweze kutumia Neno, na kufanya hivyo kwa upesi iwezekanavyo na kikamilifu. Kusaidia wanafunzi kuelewa nafasi ya maombi katika ufasiri wa kibiblia ndio lengo la sehemu hii. Hatupaswi kamwe kutenganisha upatikanaji wa hekima ya Bwana na kuiomba kutoka kwake: Yak. 1:5-6 – Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
3
M A F U N Z O Y A B I B L I A
10 Ukurasa wa 156 Maombi na Ushauri
Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online