Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 9 1

1 Fal. 3:7-9 – Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9 Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi? Mit. 3:5-7 – Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu. 8Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako Maandiko haya yanaonyesha uhusiano wa karibu kati ya kumwomba Bwana hekima, kumkiri katika njia zetu zote, na kupokea kweli yake na ufahamu wake. Kwa hivyo, usifikirie kuwa na maombi pamoja na wanafunzi wako kama jambo la kawaida sana au lisilo la lazima. Wakumbushe kila mara juu ya nafasi ya maombi katika ugunduzi halisi wa kiroho, na uwape changamoto wapate kumshirikisha Roho Mtakatifu maswali yao yanayohusiana na mawazo na kweli zinazofundishwa katika somo. Maombi ni njia ya ajabu ya kutumia kweli kwa namna ya kivitendo na yenye manufaa; kupitia kupeleka mahitaji maalum kwa Mungu kwa kuzingatia ile Kweli ya Neno la Mungu, wanafunzi wanaweza kuimarisha mawazo hayo katika nafsi zao, na kupokea tena kutoka kwa Bwana majibu wanayohitaji ili kutegemezwa katikati ya huduma zao. Bila shaka, kila kitu kinategemea kiasi cha muda ulio nao katika kipindi chako, na jinsi ulivyoupanga. Bado, maombi ni sehemu yenye nguvu na yenye uwezo wa kukutana na mafundisho yoyote ya kiroho, na kama unaweza, yanapaswa kuwa na nafasi yake kila wakati, hata ikiwa ni maombi mafupi ya yale ambayo Mungu ametufundisha, na azimio la kuishi kulingana na matokeo yake kama Roho Mtakatifu anavyotufundisha.

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online