Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

9 2 / M T A A L A WA C O R N E R S T O N E M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I

Sehemu kubwa ya kazi yako na wanafunzi ni kuhakikisha kuwa wamejitayarisha kwa ajili ya kipindi kijacho cha darasa na vipengele vyote mbalimbali ambavyo watahitaji kuwajibika navyo. Watahitaji kupitia somo na madokezo waliyoandika kwa jili ya kujiandaa na jaribio, kukariri marejeo ya Maandiko kwa ajili ya kipindi cha darasa, kusoma sehemu walizoelekezwa katika kazi ya usomaji waliyopewa, na kutoa ripoti ya kile walichogundua katika muhtasari mfupi ulioandikwa. Kwa habari ya kazi zao, wakumbushe kile kinacholengwa kimahususi katika kazi hizi. Katika masomo haya, vitabu vya kiada vinatoa ufahamu na kweli za ziada ambazo zinajaziliza maarifa yanayofundishwa katika masomo. Kazi zao za kusoma na kuandika hazikusudiwi kuwa ngumu au za kukatisha tamaa. Wanapaswa kusoma kadri wawezavyo, na kisha waandike sentensi chache juu ya kile wanachoamini vitabu hivyo vinamaanisha. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwa wanafunzi wako kujifunza, kwa hivyo hakikisha kwamba unawatia moyo katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuona hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na usisitize kwamba jambo muhimu ni uelewa wao wa kile walichosoma, si weledi wao katika uandishi. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa namna inayoharibu juhudi za kuwatia moyo na kuwajenga. Pamoja na hayo, hatutaki pia kudunisha uwezo wao kwa namna yoyote. Tafuta namna ya kuweka uwiano mzuri kati ya kuwapa changamoto na kuwatia moyo.

 11 Ukurasa wa 156 Kazi

3

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online