Mtaala wa Cornerstone, Mwongozo wa Mkufunzi

M W O N G O Z O WA M K U F U N Z I / 9 3

Ushahidi wa Agano la Kale Kuhusu Kristo na Ufalme wake Kupingwa kwa Masihi Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 4, Kupingwa kwa Masihi . Lengo la jumla la somo hili ni kuangazia na kuchambua aina ya upinzani wa kijamii na wa kiroho ambao Yesu aliukabili alipokuwa akitekeleza huduma yake ya Kimasihi katika Israeli. Kilicho muhimu kwa wanafunzi kuelewa ni asili ya migogoro kwenye huduma ya Yesu. Msisitizo huu kuhusu asili ya ushujaa wa huduma ya Yesu unapaswa kuwa mada kuu inayosisitzwa katika somo hili lote. Ukweli kwamba Yesu alikuja kunyakua mamlaka uko wazi katika Maandiko, na unapaswa kuwa msisitizo mkubwa katika mwongozo wako wa jumla wa darasa. Maandiko yaliyo hapa chini yanaweza kuwa msaada kwako katika kuwaongoza wanafunzi wako kujadili asili ya mgogoro wa kiroho ambao Yesu alikumbana nao. Mgogoro wa Kijamii Isa. 53:3 – Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Mt. 5:11 – Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Matt. 10:34-36 – Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. Mt. 10:21 – Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha. Mt. 24:10 – Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Mk 13:12 – Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha. Lk 21:16 – Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. Mt. 10:22 – Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

SOMO LA 4

 1 Ukurasa wa 159 Utangulizi wa Somo

4

M A F U N Z O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online