Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide

/ 1 1 1

M U N G U B A B A

Mungu kama Baba Wema wa Mungu

S O M O L A 4

page 295  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutoa muhtasari wa wema wa ajabu wa Mungu unaoonyeshwa katika sifa zake za kiadili za usafi, ukamilifu, na upendo wake usio na mipaka. • Kuonyesha namna usafi wa Mungu unavyoonyeshwa kupitia utakatifu, uadilifu, na haki yake. • Kufafanua sifa za Mungu zinazohusiana na ukamilifu wake, yaani, uhalisi wake, ukweli, na uaminifu wake. • Kukumbuka muhtasari wa sifa zinazohusiana na upendo wa Mungu, ukarimu wake, neema, rehema, na ustahimilivu wake. • Kueleza kwa kina msingi wa kibiblia wa ghadhabu ya Mungu kama sifa ya kiadili ambayo kwa kawaida huhusishwa na ukali wa Mungu. • Kuelezea uhusiano kati ya wema na ukali wa Mungu, upendo na haki yake. • Kuelezea uhitaji wa uelewa wa sifa na asili ya Mungu ambayo huzuia mkanganyiko au mgongano wowote kuhusu Bwana na matendo yake. Warumi 2:3-11 - Wewe binadamu, uwahukumuye wale wafanyao hayo na kutenda yayo hayo mwenyewe, je! Wadhani ya kwamba utajiepusha na hukumu ya Mungu? 4Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? 5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, 6atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; 8na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 9dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; 10bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; 11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu. Tafadhali Usijidanganye

Malengo ya Somo

4

Ibada

page 296  2

Made with FlippingBook - Share PDF online