Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 1 2 /
M U N G U B A B A
Kama lipo jambo linalowazuia watu wasiwe vile ambavyo Mungu anataka wawe ni tabia yao ya kumfanya Mungu kwa mfano wao wenyewe, kujipa uhuru uliopitiliza kwa sababu ya wema wake, kuona fadhili zake kama udhaifu, na upendo wake kama kibali cha kufanya mabaya. Hakika, “Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima, na kumjua Mtakatifu ni ufahamu,” (Mit. 9:10). Wafasiri wengi wa neno hofu au kicho cha Mungu hupunguza umuhimu wa aina hii ya kicho na hofu ya Mungu wetu aliye hai, na kufanya kicho hapa na maeneo mengine katika Maandiko kirejelee tu ile dhana nzuri ya kicho na heshima kwa Mungu. Andiko hili, hata hivyo, linaweza kufasiriwa kihalali kama woga halisi, hasira ya ndani ya moyo wa Mungu anayeonyesha fadhili zake kwetu. Fadhili hii kuu inayofurika, wema na neema ya Mungu, kulingana na Paulo katika barua yake kwa Warumi, “inakusudiwa kuwaongoza kwenye toba,” na sio kutufanya kuwa mahakimu kwa wengine au wazembe katika mwitikio wetu kuhusiana na viwango vya utakatifu wa Mungu. Utele wa fadhili na ustahimilivu na subira wapasa kutuchochea kutenda mema, kutafuta kutoharibika, kuishi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, kumwinua Masihi katika yote tufanyayo, kuwajali ndugu zetu katika Kristo, na kufanya mataifa yote kuwa wanafunzi. Kwa maneno mengine, wema wa Mungu unapaswa kukusukuma katika kutenda, kubadilisha utambuliso wako, kugeuza maisha yako. Hatupaswi kujidanganya wenyewe au kuwadanganya wengine, ufahamu wowote wa fadhili na wema wa Mungu ambao hautoi hisia za shukrani, kicho, na utayari wa kumtii Mungu ni ufahamu maskini na wenye dosari. Wema wa Mungu, kiuhalisia, hutuwezesha kunusurika na hukumu yake. Basi, na tuufurahie wema wa Mungu si kana kwamba tunastahili au tunaweza kuulipia. Tusimhukumu mtu mwingine yeyote, tukijua wazi kwamba tumeokolewa kwa sababu ya rehema na fadhili za Bwana. Tafadhali, usijidanganye. Wema wa Mungu unapaswa kukuongoza kwenye toba na badiliko, sio katika hukumu na kutimiza tamaa binafsi. Wema wa Mungu na ughubike maisha yako ili uweze kubaki mnyenyekevu, makini, na mwenye shukrani unapotafuta kutoharibika kwa njia ya imani katika Masihi. Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Wewe ni mtakatifu, Bwana, Mungu wa pekee, na matendo yako ni ya ajabu. Una nguvu. Wewe ni mkuu. Wewe ndiwe uliye juu, wewe ni Mwenyezi. Wewe, Baba Mtakatifu, ndiwe Mfalme wa mbingu na nchi. Wewe ni Watatu na Mmoja, Bwana Mungu, mwema
4
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook - Share PDF online