Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
/ 1 1 3
M U N G U B A B A
hasa. Wewe ni mwema, Mwema hasa, Mwema mkuu, Bwana Mungu, uliye hai na wa kweli. Wewe ni upendo, wewe ni Hekima. Wewe ni unyenyekevu, wewe ni ustahimilivu. Wewe ni pumziko, wewe ni amani. Wewe ni furaha. Wewe ni haki na kipimo cha kiasi. Wewe ni utajiri wetu wote, na unatutosha. Wewe ni mzuri. Wewe ni mpole. Wewe ni mlinzi, wewe ni mlezi na mtetezi wetu. Wewe ni ujasiri. Wewe ni kimbilio na tumaini letu. Wewe ni imani yetu, faraja yetu kuu. Wewe ni uzima wetu wa milele. Bwana mkuu na wa ajabu, Mungu Mwenyezi, Mwokozi wa rehema. ~ St. Francis wa Assisi, 1181-1226.
Appleton, George, mhariri. The Oxford Book of Prayer. Oxford; New York: Oxford University Press, 1988. uk. 62-63
Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 3, Mungu katika Utatu: Ukuu wa Mungu.
Jaribio
Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Mathayo 3:16-17.
Mazoezi ya kukariri maandiko
Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).
Kazi za kukusanya
4
MIFANO YA REJEA
Uhuru au Rukhsa?
Kanisa zima limesisimka baada ya mfululizo wa somo la asili ya neema ya Mungu katika Kristo lililofundishwa na mchungaji wa vijana. Fundisho lake la kibiblia na la wazi kuhusu neema ya Mungu lilipokelewa vema, na alieleza vema kwa vijana kuhusu uhuru wetu katika Kristo dhidi ya sheria, nguvu ya asili ya dhambi ya kale, na majaribio yote ya kimwili ya kumpendeza Mungu bila damu ya Kristo. Watoto wachache, baada ya kusikia kwamba hawakuhitaji kufanya lolote ili kupata kibali cha Mungu, wameanza “kuonyesha uhuru wao” katika namna ambazo zinaonekana kwa baadhi ya watu kanisani kama rukhsa kuliko uhuru katika Kristo. Wameanza kuvaa “kidunia,” kuleta muziki wa kidunia katika ukumbi wa ibada, na wanataka kucheza mitindo mbali mbali kanisani. Wengine wanadhani ni jambo zuri la ajabu,
1
Made with FlippingBook - Share PDF online