Mungu Baba: Swahili Module 6 Mentor Guide
1 1 4 /
M U N G U B A B A
huku wengine wakimlaumu mchungaji wa vijana kwa kuingiza mawazo haya ya kidunia kuhusu uhuru katika akili za watoto. Je, unashughulikiaje suala hili ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa kile ambacho uhuru wa Kristo unamaanisha hasa kama mwitikio kwa wema wa Mungu?
“Kuwaogopesha Watu Hakuleti Matokeo.”
Mshirika mmoja ambaye kwa muda mrefu amekuwa sehemu ya kusanyiko siku moja alitoa maoni yake kwa mchungaji, “Nimekuwa nikikusikiliza kwa miaka minne sasa, na sidhani kama nimewahi kukusikia ukifundisha kuhusu ghadhabu ya Mungu. Namaanisha haujawahi kufundisha katika mafundisho ya Biblia, mahubiri, warsha, semina – hakuna popote. Najua pengine panaweza kuwa na sababu nzuri kwa hili, lakini kwa nini hutaki hata tu kuitaja? Biblia hakika inafanya hivyo!” Mchungaji alimwitikia mshirika huyu kwa kichwa, na akajibu, “Uko sahihi, sijawahi kuhubiri kuhusu hili tangu niwe hapa. Siamini tu kwamba kufundisha ghadhabu ya Mungu kunawasaidia watu kuelewa kiuhalisia nia ya Mungu ni nini leo. Kristo alikuja kuokoa, si kuhukumu, na watu wanahitaji kujua kuwa Mungu anawajali, na sio waogopeshwe na kuja kwa Yesu kwa sababu ya hofu. Kusema kweli, kupitia huduma yangu kwa miaka mingi, kama lipo jambo moja nimewahi kujifunza ni kwamba kuwaogopesha watu hakuleti matokeo. Watu hawahitaji kutishwa ili waamini; badala yake, wanahitaji kupendwa ili waamini.” Je, unakubaliana na tathmini ya mchungaji huyu ya kazi yetu ya kuwaeleza watu kuhusu upendo na ghadhabu ya Mungu? Ni wapi yuko sahihi na wapi amekosea? Akitoa maelezo ya sababu iliyomfanya ashindwe kuwa Mkristo, mfanya kazi mwenzako anakuambia wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana, “Ninampenda Yesu na mazungumzo yote kuhusu upendo na kila kitu, lakini jambo nililogundua ni kwamba Wakristo wengi ni watu wakorofi sana. Wanapinga mambo mengi sana, wanachukia kila aina ya vikundi, na wanaonekana tu kutokubalika kuhusu mambo mengi. Na, nikitazama namna walivyowatendea baadhi ya wainjilisti maarufu walioanguka, ni kama kuwashambulia kwa risasi majeruhi wao wenyewe. Pamoja na maongezi yao yote kuhusu neema na wema wa Mungu, wao hawaonekani kuwa na fadhili kwa yeyote, na hawaoni lolote jema katika chochote. Nisingeweza kuwa Mkristo. Ni wakorofi sana!” Je, ungemjibuje mtu huyu mwenye mtazamo wa namna hii kuhusu kushindwa kwa Wakristo kuakisi neema ya Kristo? “Wakorofi Sana”
2
4
3
Made with FlippingBook - Share PDF online